January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Matukio yaliyosisimua

Wanakijiji wakijaribu kumkabili ng’ombe dume wakati wa sherehe za mavuno maarufu kama Jallikattu ambayo huwa inasherehekewa kwa namna yake huko Kusini mwa India mjini Madurai uliopo Jimbo la Tamil Nadu juzi. (Picha na REUTERS).

Watoto wakiwa wanacheza ndani ya hema la kulala ambalo limezingirwa na maji machafu katika moja ya kambi za wakimbizi wa ndani ya Umm Jurn katika Kijiji cha Kafr Uruq nchini Syria juzi. Taifa hilo linaendelea kukabiliwa na mizozo ya muda mrefu ambayo imeathiri mamilioni ya raia. (Picha na AFP).
Wahamiaji raia wa Honduras wakikabiliana na maafisa wa usalama wa Guatemala katika eneo la Vado Hondp nchini humo wakati wakishinikiza kupita kwa nguvu kuingia nchini Marekani, Januari 17, 2021. Maafisa usalama wa Guatemala walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya maelfu ya wahamiaji hao. (Picha na AFP).
Rais wa Marekani,Joe Biden akimkumbatia Mke wa Rais Jill Biden baada ya kuwasili rasmi katika Ikulu ya White House juzi mjini Washington muda mfupi baada ya kula kiapo. (Picha na AFP).