April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Marioo alamba dili la Ubalozi Partmatch

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mchezo wa ubashiri ya Parimatch imemtangaza rasmi Msanii wa Bongofleva Omary Ally maarufu kama “Marioo” kuwa balozi wa Kampuni hiyo ili kuwakutanisha mashabiki wake katik michezo ya ubashiri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch Erick Gerald alisema ujio wa Marioo umekuwa mzuri kwani kwa sasa Parimatch ndio Kampuni namba moja ya ubashiri ikiwa na ofa za kijanja na tovuti yenye muonekano mzuri.

“Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Marioo kama balozi wetu kwa ajili ya kuzidi kupata burudani, hivyo Marioo amepambana na ameweza kufanya vizuri huwezi kuongelea Muziki wa Bongofleva bila kumtaja Marioo,” alisema Gerald.

Hata hivyo, alieleza namna ubalozi wake utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza wateja wapya pamoja na kusaidia kutoa uelewa kwa wachezaji hasa ya kubeti ili wote waweze kushinda.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Emmanuel Ndaki aliwapongeza Kampuni ya Parimatch kwa kuunganisha tasnia ya muziki kuwa sehemu ya Michezo ya ubashiri.

“Ni hatua kubwa kwa Kampuni ya Parimatch kuona juhudi za wasanii wa muziki wa Bongofleva kuingia kwenye Michezo na kuleta hamasa kubwa kuendelea na mchezo wa kubashiri, kuongeza pato la taifa na kuhakikisha mchezo huu unakua wa kistaarabu,” alisema.

Kwa upande wake Msanii wa Bongofleva Omary Ally Mwanga aliushukuru uongozi wa parimatch kumkaribisha kwenye familia yao kwani ni Kampuni ambayo ni kinara wa Michezo ya ubashiri mtandaoni.

Marioo mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa balozi wa Kampuni hiyo kwa muda wa mwaka mmoja ,alisema kutokana na ushawishi wake kwenye tasnia ya muziki ana amini pia ana mashabiki wengine kwenye Michezo ya ubashiri.

“Kutangazwa kwangu kuwa balozi naenda kuunganisha mashabiki zangu wa Michezo ya kubashiri na burudani kuwa sehemu moja,” alisema Marioo.

Marioo alisema namna fursa hiyo ya parimatch inaenda kumkutanisha kwenye michezo ya ubashiri na kwa sasa ni muda mzuri ambapo kombe la dunia nchini Qatar ambapo watu wengi watatupia ubashir wao Parimatch.