May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Rais wa Marekani kutembelea Tanzania

Na Penina Malundo, timesmajira

MAKAMUĀ  wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajiwa kutembele Tanzania kuanzia Machi 29 hadi 31, 2023, kufuatia mwaliko wa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo inakuwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi za Bara la Afrika .

Ziara hii inafanyika takriban miezi 11 tangu viongozi hawa wawili wanawake walipokutana Ikulu ya Marekani na kubadilishana mawazo juu ya majukumu ya katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani uliodumu kwa miongo mingi tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,ilisema kwenye ziara hiyo,Makamu huyo wa Rais wa Marekani Kamala anatarajia kukutana na Rais Dkt. Samia na kufanya nae mazungumzo,kupata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kukutana na vijana wajasiriamali wa Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hiyo ilisemaĀ  ziara hiyoĀ  ya Kamala,nchini Tanzania inaleng kuongeza nguvu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania hususan baada ya kufanyika kwa mkutano kati ya Marekani na nchi za Afrika maarufu kama US – Africa Summit mwezi Disemba 2022, ambapoĀ  Dkt. Samia alihudhuria.

Aidha ilisema ziara hiyo ni ya kihistoria ambapo Makamu wa Rais wa Marekani ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo, anafanya ziara ya kikazi Tanzania na kukutana na Dkt. Samia ambaye pia ni Rais wa kwanza mwanamkeĀ  wa Tanzania.

Mbali na Makamu huyo Kamala kukutana na Rais Dkt Samia kwa mazunghumzo pia ziara inalenga katika kuunganisha nguvu za ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi Tanzania na Marekani katika sekta za afya, kilimo, utalii, uchukuzi, uchumi wa buluu, mawasiliano, uchumi wa kidijitali, uungaji mkono hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uhimilivu wake na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kupitia ubunifu, ujasiriamali na uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu ambazo Makamu huyo wa Rais nchini Marekani, na ujumbe wake watazitembelea ndani ya bara la Afrika kuanzia MachiĀ  25Ā  hadi tarehe 2 Aprili 2023 huku nchi nyingine zikiwa niĀ  Ghana na Zambia.