April 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahundi akichangia milioni 5 kikundi cha Mwanamke Shujaa

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline, Rungwe

KATIKA kuhakikisha wanawake wanajikomboa kiuchumi katika nyanja mbalimbali za kuachana na dhana ya kuwa tegemezi,Naibu Waziri wa maji ambaye pia Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi amezidi kuyafikia makundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi .

Kikundi kimojawapo kilichofikiwa na mkono wa kheri ni kikundi cha Mwanamke Shujaa cha Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambacho kimechangiwa Mil.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya kufugia mifugo .

Mhandisi Mahundi katika hafla hiyo ya maadhimisho ya sikukuu ya wanawake alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya Tukuyu mjini ambapo lengo lilikuwa kupata mil.20 ili waweze kufikia malengo .

Mahundi amechangia zaidi ya mi.3 akiwa ameungwa mkono na rafiki zake.

Lengo la Mahundi ni kuhakikisha wanawake wanamiliki uchumi wao akitekeleza kauli mbiu yake ya “Twende Tukue Pamoja”