Na Mwandishi Wetu, TimesMajira ONline
MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalengo, Maalim Seif Sharif Hamad leo amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais visiwani Zanzibar kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Viongozi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Maalim Seif amekabidhiwa fomu hiyo leo na Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu katika ofisi za Chama za Vuga Zanzibar.
Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni baadhi ya wanachama wa chama hicho walijitokeza na kumabidhi kiongozi huyo fedha walizomchangia wakitaka azitumie kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
More Stories
Bodi ya NHIF yatakiwa kutatua changamoto za wanachama wake
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima