May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Moja ya Pikipiki aliyobuni Mwanafunzi wa Chuo cha Veta. Dodoma, Simon Njovu kwa lengo la kusaidia usafiri kuwa rahisi zaidi. Picha na Penina Malundo, TimesMajira Online

Veta Dodoma yawataka vijana kujifunza ufundi

Moja ya Pikipiki aliyobuni mwanafunzi wa Chuo cha Veta. Dodoma, Simon Njovu kwa lengo la kusaidia usafiri kuwa rahisi zaidi.

Na Penina Malundo, Timesmajira Online

CHUO cha Ufundi Stadi (Veta) Mkoa wa Dodoma, kimetoa wito kwa vijana nchini kuacha kukaa mtaani badala yake kujikita na mafunzo ya ufundi ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

Mwalimu wa Chuo hicho Dodoma, Dayosta Mshori amesema hivi sasa vijana wanapaswa kujitoa na kujituma ili kuweza kufanikiwa katika maisha yao na ndio maana Chuo cha Veta kimekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia vijana katika kuwainua kifani na kuwafikisha sehemu ambayo wanaweza kujisimamia.

Amesema, kwa muda mrefu wamekuwa wakiwapokea vijana wakiwa ngazi ya chini na kuwaelekeza fani mbalimbali ambazo baadae wanakuja kuchagua zile zinazowafaha katika kujifunza zaidi.

“Tunawajengea uwezo vijana kujifunza katika mafunzo mbalimbali na tukigundua kama wanakipaji cha ubunifu tunawasaidia kuwaendelezea kutimiza ndoto yao. Tayari tunao baadhi ya vijana ambao tumewasapoti akiwemo Mbunifu wa Pikipiki iliyotumia mashine ya kumwangilia na baadhi ya vifaa vya baskeli ambayo veta imemsaidia hadi kuikamilupisha,” amesema

Kwa Upande wake Mbunifu wa Pikipiki hiyo, Simon Njovu amesema mwanzo alipokuwa anaingia Veta kupata mafunzo aliona fursa ya kutumia ubunifu wa kutengeneza kifaa cha usafiri Pikipiki ambayo ametengeneza kwa kutumia vifaa vya hapa hapa nchini na zinauwezo wa kumsaidia mtu katika safari zake.