May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maadhimisho siku ya walimu Duniani ni kila baada ya miaka 4

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

AFISA Utumishi wa Chama cha walimu Taifa CWT Neema Ezekia Amesema maadhimsho ya siku ya walimu Duniani Kwa utaratibu wa Chama hicho taifa yanafanyika kila baada ya miaka minne na mwaka huu yalikuwa yafanyike Novemba 4,2023 Kwa ratiba iliyokuwa imepangwa.

Amesema kuwa maadhimisho ambayo yamefanyika katika ngazi za Wilaya ni Kwa utaratibu ukizingatia siku hiyo ni siku ya walimu Duniani lakini kitaifa lazima yaadhimishwe kitaifa na yaratibiwe na ngazi ya juu ya Chama hicho.

Neema ameyasema hayo Disemban 8 ,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi kuhusu Malalamiko na shutuma zinazoletwa na baadhi ya walimu na wanachama waChama hicho.

Amesema kuwa wao kama Chama taifa hakiwezi kuwafunga walimu kufanya sherehe hizo kwenye ngazi za wilaya Kwa lengo la kusubiri sherehe ya ngazi ya kitaifa ila kile ambacho linakwenda kufanyika katika maadhimisho hayo basi hata hao walioadhimisha watakuwa ni miongoni mwa watakaoshiriki.

Akizungumzia Wilaya ambazo zilifanya maadhimisho hayo ya siku ya walimu Duniani ni kagera,kibiti ,Tanga jiji na kisarawe, hivyo msukumo mkubwa wa kufanya maadhimisho hayo nikwasababu pia wanatukio moja kubwa sana la kutimiza Kwa miaka 30 ya Kuzaliwa Kwa Chama cha walimu nchini CWT.

“Chama hiki kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake hivyo kupitia maamuzi yaliyotokana na vikao vya ndani ambapo yalikuwa nikufanya matukio hayo mawili Kwa wakati mmoja na ndio maana wao wamekuja na maandalizi ya siku ya mwalimu Duniani lakini kikubwa ni maadhimisho ya miaka 30 ya Chama “Amesema Neema

Nakuongeza kuwa “Chama cha walimu sio chombo kidogo ni chombo kikubwa sana na jambo hili tunaliandaa katika ubora wake Kwa maana ya kubeba taswira nzima ya Chama kama kilivyo na si vinginevyo ” amesisitiza

Kuhusu taarifa za uwepo wa ufisadi ndani ya Chama Afisa Utumishi huyo Amesema ni mambo ya ajabu kwani tukio lenyewe halijafanyika lakini wanashangaa kusikia baadhi ya watu wanazungumzia ufisadi kimsingi hakuna jambo ambalo linaweza kufanyika pasipokuwa na maandalizi ila ieleweke kwamba jambo hilo nikubwa na matarajio ya maadhimisho hayo nikuwa na mgeni rasmi ambaye ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Dhana au taswira ya kuzungumzia ufisadi basi lipatikane baada ya shughuli nzima kukamilika kwasababu hapa siwezi kuzungumza nikatika maeneo gani ambao huo ufisadi unafanyika lakini tunalifanya Kwa uratibu ambao uko wazi na mipango yote inaanzia kwenye vikao.”Amesema

Amefafanua kuwa jambo hilo wanalokwenda kulifanya ni jambo kubwa na wanakusudia kushiriki walimu takribani 40,000 na walimu wapo tayari kuhudhuria na mwitikio ni mkubwa sana lengo nikuona hadhi ya siku ya mwalimu inafikiwa na wao kama Chama taifa nikuhakikisha wanaratibu na kufanikisha kufanyika Kwa tukio hilo.

Hata hivyo Rais wa Chama cha walimu Tanzanaia CWT Leah Ulaya Amewataka walimu wote nchini kupuuza taarifa za upotoshaji zinazoendelea kwani maadhimisho hayo yameratibiwa na vikao halali vya Chama cha walimu Tanzanaia.

“Kwahiyo Kila mmoja anafahamu kwenye vikao hivyo tuna uwakilishi wa kutosha katika maamuzi Kila mkoa tumepta wajumbe takribani saba na hao Saba wanaporudi mikoani kwao wanakwenda mpaka wilayani kutoa taarifa.”Amesema

Nakuongeza kuwa .”bahati nzuri maadhimisho haya yamekubaliwa na nakuratibiwa Baraza kuu la Taifa ambapo chombo hicho ndio chombo pekee kinaratibu na kupanga bajeti za Chama.

Pia ameongeza kuwa Katika maadhimisho hayo wanatarajia mgeni rasmi kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo wao kama Chama wanapanga jambo la kuwasilisha mbele ya mkuu wa nchi.

Amesema kuwa anaamini uwepo wa mh.Rais Dkt Samia utatoa nafasi Kwa rais kuzungumza au kuelekeza mambo mbalimbali ya kielimu na hata Kwa jamii ya watanzania wote