April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kundi maalum watumiaji bidhaa za Apple kuzinduliwa

Na Idd Lugengo, TimesMajira,Online,Dar

KAMPUNI ya IStore inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa ya ‘Apple’ imetangaza kuzindua kundi maalumu la watumiaji wa bidhaa hizo nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa IStore kundi hilo litawawezesha watumiaji wa bidhaa za ‘Apple’ kukutana na kutengeneza urafiki na watumiaji wengine wa bidhaa hizo pamoja na kuuliza maswali na kupata majibu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu bidhaa hizo.

Wakizungumza na TimesMajira,Oline jana wamiliki wa IStore wamesema kundi hilo litajumuisha watu wa rika zote, wenye uelewa wa kati kuhusu kompyuta, wataalamu wa kompyuta na wengine kutoka katika fani na taaluma mbalimbali.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa la watumiaji wa bidhaa za ‘apple’ nchini Tanzania haswa simu za I phone, na kupelekea kutanuka kwa matumizi ya bidhaa hizo hapa nchini.