May 11, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kukithiri kwa utoro na wanafunzi kuacha shule kwawachefua Madiwani na Dc Kyela

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Kyela,

WIMBI la utoro na kuacha shule wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari wilayani Kyela mkoani Mbeya kukimbilia kwenye biashara ya Cocoa kwawaibua madiwani wa halmashauri hiyo na kuamuru wazazi waeleze sababu za wanafunzi kuacha shule kiholela bila sababu za msingi.

Imeelezwa kuwa kikombe kimoja cha Cocoa ni shilingi,6000 hivyo watoto wanaona bora wakaibe cocoa za watu na kuuza ili apate sh.6000 huku wakiacha elimu ambayo ni muhimu hivyo wanaenda kuzalisha panya road ambao watakuwa wezi.

Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha baraza la madiwani wilayani Kyela wakati Mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya,Adamu Kabeta ambaye ni Diwani wa Kata ya Busale baada ya kuwasilisha ya taarifa ya kamati ya elimu afya katika kikao hicho.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa suala la kuacha Shule watoto ni suala mtambuka ambalo linaweza kusababishwa na mambo mbalimbali ya kimaradhi na vitu vingine kama kamati walikubaliana kuwa hawataki kusikia utoro wala mimba katika Shule na labda mtoto aache shule kwa maradhi ama kifo .

Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo iliibuka hoja kutoka kwa Diwani wa Kata ya Matema wilayani humo, Antony Mwamgunda amesema kuwa Rais Samia anajitahidi Sana kuleta maendeleo lakini huku watoto hawasomi hili ni tatizo kubwa liangaliwe Sana na uongozi wa wilaya.

Amewaomba viongozi wa dini hili jambo walihuburi kwa ajili ya watoto wetu wilaya ya Kyela kizazi kinakwenda pabaya kimemuacha Mungu .

Akielezea zaidi Diwani Mwamgunda amesema kuwa hata Ilani ya chama cha mapinduzi wamezungumzia elimu ambayo madiwani wanasimamia pamoja na CCM.

Diwani mwingine Kata ya Mwaya ,Ackimu Mwanyilu amesema kuwa wapo kwenye suala la elimu kutosoma Shule na utoro mashuleni ni jambo ambalo linasikitisha Sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania chini ya Rais Samia inajitahidi kuhakikisha miundombinu ya shule inakuwa vizuri lakini ajabu yake baadhi ya watoto wanashindwa kusoma shule kama madiwani na Wananchi tunaomba hii tabia ikomeshwe.

“Hii tabia tunaomba ikomeshwe kwasababu kijana yeyote anatakiwa apate elimu ili awe kuwa kiongozi wa Taifa hili,naiomba serikali ijitahitadi kuthibiti hawa watoto ambao wamekuwa watoro shule”amesema Diwani huyo.

Akichangia mjadala huo Mwenyekiti wa halmashauri ya Kyela na Diwani kata ya lkimba Katule Kingamkono amesema kuwa kuna Shida kubwa kwenye halmashauri ya Kyela kwasasa hivi wazazi hawalichukulii uzito suala la elimu .

“Sisi Wana siasa ni wana siasa tu Sasa ikitumika nguvu ya dola inaweza kutusaidia na tusipoliangalia hili tunaweza kuzalisha kizazi kibaya hapo baadaye tuombe hili mh Dc utusaidie na mkurugenzi utupe takwimu sahihi hali sio nzuri hivyo tunaamini mamlaka zote zikishikamana mh Dc unaweza kutusaidia tuna wimbi kidogo ambalo tusipoliwekea nguvu tutakuwa na kizazi kibaya kwasababu sasahivi mzazi anakwepa Nini vitu vingi serikali inabeba majukumu mengi ikiwemo miundombinu ya shule kuwa mizuri lakini watu wanaona kuacha Shule ni sawa tu”amesema Mwenyekiti huyo.

Mkuu wa wilaya ya Kyela, Josephine Manase amekiri kuwepo kwa utoro mashuleni na kusema watoto wote walioacha Shule bila sababu za msingi na bila taratibu zinazotakiwa wanaenda kufanya msako na kuwa humiliation hatua,mh Rais Samia amefanya kazi kubwa ya kujenga madarasa ya kisasa na kuboresha miundombinu ya shule.

Mwalimu Kanzale Mwangungulu ni Kaimu ofisa elimu msingi na awali amekiri kuwepo kwa tatizo la kuacha Shule watoto na utoro na kusema kuwa asilimia wanafunzi watoro linapatikana zaidi Shule ambazo zipo mpakani ambazo ni Katumba Songwe,Kasumulu na sehemu zingine familia zinaingiliana kuna wengine wanaishi Tanzania na wengine Malawi kipindi cha likizo mara wanafunzi wanaenda likizo kwa wazazi wa upande mmoja.