April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mji wa Kigoma

Kigoma yaendelea kupambana na Corona

Na Mwajabu Kigaza, Kigoma.

MKOA wa Kigoma katika kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu COVID 19  hadi sasa jumla ya watu 47 wakiwemo wafanyabiashara 27 wanaotumia usafiri wa maboti kusafirisha shehena za mizigo kuelekea nchi ya kidemocrasia ya Congo DRC na Burundi wamewekwa katika Karatini kwa muda wa siku kumi na 14.

Akizungumzia hilo wakati akitoa taarifa kwa  Mkuu wa mkoa  Kigoma kuhusu hali ya udhibiti wa wasafiri wanaoingia nchini Mganga Mkuu wa manispaa ya kigoma Ujiji, Sebastian Siwale alisema wafanyakazi hao wa maboti kati yao wapo manahodha 11 wa boti naneyza mizigo ambayo inafanya safari zake katika nchi za Congo na Burundi na kwamba hadi sasa kuna vituo vitatu ambavyo vimeteuliwa kwa ajili ya kuwahudumia wasafiri wanaotoka nje ya nchi ambao wanatakiwa kukaa karantini.

Viongozi wa chama cha wamiliki wa maboti Kigoma na wasafirishaji wa shehena UWAMAKI walisema kuwa kuwekwa karantini siku 14 kwa watumishi wa boti  zinazoenda nje ya nchi kumeleta athari kubwa kwao kiutendaji kwani inachukua muda mrefu kwa boti kufanya tena safari zake kwenda nje ya nchi hata kama shehena ipo tayari.

Mwenyekiti wa chama hicho, Edmund Msabaha alisema kuwa pamoja na kuchelewa kusafirishwa kwa shehena pia chama kinalazimika kugharamia matunzo ya familia za mabaharia hao kwa siku zote wanapokuwa karantini jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa wamiliki wa maboti na wasafirishajiwa shehena.

Hata hivyo wamiliki hao walitoa maombi la kutaka eneo la bandari ndogo ya Kibirizi kuwe na karantini lakini pia kutaka muda wa kukaa karantini upunguzwe kutoka siku 14 hadi siku saba ambapo kamati ya ulinzi na usalama mkoa ambayo ilifika kukagua eneo hilo imeeleza kutoridhishwa na eneo hilo.

Akitolea ufafanuzi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, mara baada ya ukaguzi wa eneo hilo na kujiridhisha kwamba eneo hilo halifai kutokana na kukosekana kwa  miundombinu ya kutosha kwa ajili ya watu wanaoingia kutoka nchi jirani kwa kutumia usafiri wa boti kuwekwa karantini ambapo pia alitaka kuongezeka a umakini kwa wale waliowekwa karantini ili kudhibiti wale wanaotoroka.

Afisa wa Bandari ya Kigoma, Theodry Lutandula, ameeleza utaratibu unaotumika wa kuwaweka karantini wasafiri wanaowasili bandarini hapo kwa kutumia meli zisizokuwa na miundombinu ya huduma za kijamii kuwa ni pamoja na kuhakikisha wasafiri wote wananawa mikono mara baada ya kutoka katika chombo cha usafiri lakini pia wanafanyiwa vipimo lakini pia kutumia dawa kupulizia katika meli.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr Simon Chacha, amewapa maelekezo wasafirishaji wa maboti kupunguza idadi ya watu wanaosafiri kwa kutumia usafiri wa boti ambapo alisema ni lazima kuwe na utaratibu wa kuwa na mabadiliko kwa wale ambao wanahusuka katika vyombo vya usafiri.

“ inatakiwa kuwe na makundi mawili wengine wakienda na kurudi wanawekwa karatini na halafu kundi linguine nalo linaenda likirudi hao walioko karatini wamelaliza muda wao nao wanaenda hili litasaidia kuendelea shughuli za usafiri na usafirishaji wa mizigo” alisema