March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kesi ya Sheikh dhidi ya
Nabii Suguye yaahirishwa

Na Rose Itono, Timesmajira Online

UTETEZI wa kesi ya madai ya kuvamia kiwanja kinachodaiwa kumilikiwa na Rais wa Jumuiya inayojishughulisha na usafitishaji wa mahujaj ya Al Jazira International Haji Trust,Shekhe Al Amin Juma inayomkabili Nabii Nicolaus Suguye imeahirishwa kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kuwa na majukumu mengine.

Kesi hiyo imeahirishwa na Baraza la Ardhi la Wilaya ya Ilala, ambapo mlalamikiwa Nabii Suguye anatoka kanisa la The World of Reconciliation lililopo Kivule.

Akiahirisha kesi hiyo leo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mwendwa Mgulambwa amesema kesi itaendelea Juni 14, mwaka huu kwa mdaiwa kujitetea kwa kuwa Mwenyekiti anayesikiliza shauri hilo ana kazi zingine.

Kesi hiyo ambayo mtoa maombi Shekhe Juma anawakilishwa na Wakili Sypriano Silungwe alikubaliana na Mwenyekiti ambapo tayari upande wake umeshatoa ushahidi

Silungwe amesema upande wa mtoa maombi ulikuwa na mashahidi watatu, akiwepo mtoa maombi.

Utetezi wa mtoa maombi mahakamani hapo amedai kuwa alinunua kiwanja hicho cha ekari kumi eneo la Bangulo Kata ya Pugu mwaka 1996 wakati huo kulikuwa bado shamba

Shekhe Juma amesema aligundua robo tatu ya ekari moja ya kiwanja chake kimevamiwa mwaka 2017 baada ya kurudi kutoka kwenye matibabu nchini India

“Baada ya kutoka India kwenye matibabu mwaka 2017 nikagundua robo tatu katika heka moja ya kiwanja changu kimevamiwa na kujengwa vibanda ndipo nikachukua hatua za kisheria kwa kuweka zuio”,amesema Shekhe Juma.

Ameongeza kuwa mara kadhaa mvamizi wa kiwanja alimfuata na kumuomba amuuzie, jambo ambalo hakukubaliana nalo na ndipo kesi ilifikishwa mahakamani

Mdaiwa katika shauri hill anawakilishwa na wakili Christine Katala. Kesi hiyo itakuja tena Juni 14 kwa utetezi