May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu ,Zanzibar awapa maua yao NSSF na Serikali itaendelea kuwasapoti

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ( Zanzibar ) Fatma Hamad Rajab akiwa katika banda la NNSF katika maonyesho ya madinni mkoani Geita

Na David John Timesmajira oniline,Geita

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ( Zanzibar ) Fatma Hamad Rajab amewapongeza mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kwa kazi kubwa wanayoifanya na wao kama Serikali wanahakikisha waendelea kushirikiana bega Kwa bega na Mfuko huo ili kuhakikisha wanaitangaza NSSF maeneo yote kama ambavyo waliweza kufanya kisiwani Pemba na hatimaye kupata wateja wengi.

Katibu Fatma ameyasema hayo septemba 22 nwaka huu wakati akitembelea banda la Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) kwenye Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini iliyoambatana na kauli mbiu isemayo ” Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira”

Amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na Mfuko NSSF Kwa lengo la kuwapatia wateja weng zaidi na huku akiwaapongeza watumishi wa mfuko wa hifadhi za jamii ( NSSF ) Mkoa wa Geita chini ya Meneja wake Winniel Lusingu kwa uwajibikaji wao katika kuwatumikia wateja wao.

” Nitashirikiana nanyi ili kuhakikisha NSSF inapata wateja wengi zaidi kama ambavyo waliweza kufanikiwa kisiwani Pemba na tukapata wateja wengi zaidi ambao sasa hivi wanakwenda Dar es salaam au Tanzania kutafuta nyumba na Viwanja, lakini pia nitahakikisha watu wengi wanajiunga na Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) hadi kieleweke” amesema Fatma.

Pia amewapongeza watumishi hao kwa kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na upendo, hakika mnapiga kazi nzuri sana, na kinachosababisha ni umoja wao nanhivyo kuwataka kuendelea kuwa wamoja, lakini pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanampa nguvu Mkurugenzi wao ili aweze kufanya kufanya kazi nzuri zaidi na zaidi ili kuhakikisha NSSF inaendelea kufanya vizuri.

” Muwe karibu sana maana mie kwani mimi ni lulu, dhabhabu, hivyo hiyo Dhahabu muwe nami karibu sana ili kuhakikisha kazi zote zinakwenda vizuri,lakini mnasaidiana katika matukio yote ikiwa ya kazi, kijamii hakikisheni mnashirikiana ili kuhakikisha wote mnafanya kazi kama timu ya pamoja” amesema Katibu Mkuu Fatma.

Kwaupande wake Meneja wa Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) Mkoa wa Geita Winniel Lusingu amesema Mfuko huo unaangalia Sekta binafsi na Sekta isiyo rasmi, hivyo kuwepo kwenye Maonyesho hayo wako kwa wadau wao muhimu .

” Kuwepo hapa kwenye Maonyesho haya kwa kweli ni wadau wetu ambao wanatusaidia kwa kiasi kikubwa sana cha mchango, kwani Ofisi ninkama imehamia hapa , wanacha wakija hapa wanapata huduma zote kama wako Ofisini, lakini kwasababu NSSF tumeenda mbali zaidi Kiiteknolojia tunahakikisha kwamba wanachama wetu popote wanapo kuwepo wanaweza kupata huduma za NSSF kikamilifu nankwanurahisi zaidi” amesema Winniel Lusingu.