Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online
IMEELEZWA kuwa kupitia Kampeni ya Mchanga Pekee inayofanya usafi pembezoni mwa eneo la bahari hususani katika fukwe ya Coco,imebaini kuwepo kwa idadi kubwa ya vipande vya chupa za plastiki , pini, sindano, vifuniko vya chakula, majani, vifungio vya plastiki, mifuko ya kubeba plastiki pamoja na makombo ya chakula kutoka kwenye takataka .
Uchafu huo unatokana na jamii kutokuwa makini katika utunzaji wa mazingira na badala yake kutupa ovyo takataka pasipokuweka katika vyombo maalum vya kuhifadhia taka.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Mawasiliano wa Kampuni ya Coca-Cola Kwanza,Haji Ally Mzee ,amesema asilimia kubwa ya taka za baharini zinatoka pwani kupitia mito , mifereji ya maji na fukwe ambapo inakadiriwa kuwa kila kilomita ya mraba ya bahari ina vipande 13,000 vya vifaa vya taka za plastiki.
Amesema kila mwishoni mwa wiki, fukwe hiyo ya Coco hupokea wastani wa watu 300 hadi 500 kwa nyakati tofauti ambapo wamekuwa wakiwasisitiza na kuwakumbusha uhifadhi mazingira kwa mustakabali wao na vizazi vijavyo.
“Hivi sasa, zaidi ya watu 5,000 wanaokuja katika maeneo hayo wameelimika na kufanikiwa kutumia vyombo maalum vya taka, kutupa taka baada ya matumizi,”amesema na kuongeza
“Kupitia kikundi chao cha kusafisha pwani, makadirio ya chupa za plastiki 150, zaidi ya vifungashio 250 vya plastiki ni idadi kubwa ya uchafu wa baharini ambao ulihamia pwani na mawimbi yenye nguvu ya bahari zilikusanywa,”amesema
Mzee amesema chupa za plastiki zinazokusanywa husafirishwa moja kwa moja kwa wazalishaji wa chupa za plastiki kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa za plastiki nyingine.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya