May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kairuki mgeni rasmi tamasha la KCF

Na Mwandishi wetu

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii ,Angels Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la Kilimanjaro cultural Festival litakalofanyika Desemba 27 na 28 viwanja vya Kilihome Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamessemwa na Mwenyekiti wa Kilimanjaro Cultural Festival (KCF) Jana,Ansi Mmasi,wakati akiongea na waandishi wa habari  amesema tayari maandalizi ya tamasha hilo,yamekamilika, na hakuna kiingilio chochote.

Amesema Waziri Kairuki atapata fursa ya kuzindua program maalum ya homestay inayotoa fursa kwa wananchi wa Kilimanjaro kujisajili na kuruhusu nyumba zao zitumike kwa malazi ya wageni watakaofika kwa shughuli mbalimbali za utalii na kutembelea vivutio vilivyopo Mkoani Kilimanjaro.

“Natoa wito kwa Wananchi kujitokeze kwa wingi Kilihome kushuhudia mambo mengi mazuri yatakayoimarisha na kuelimisha kuhusu Mila, tamaduni na desturi pamoja na kufahamu vivutio vya asili vilivyopo Kilimanjaro,”amesema na kuongeza 

“Pia Waziri Kairuki atakabidhi zawadi kwa vikundi vya washindi wa ngoma za asili na watoto wa umri wa Kati ya miaka 19 hadi 18  waliofanya vizuri kwenye shindano la kuzungumzia vivutio vya asili katika maeneo yao kwa lugha fasaha za asili za makabila yao,”amesema.

Mmasi amesema siku ya kwanza ya tamasha litakalofunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, timu ya msafara wake itatembelea mapango ya asili ya Chagga curve yaliyopo Marangu na msafara mwingi utaelekea Kibosho Kirima kutembelea mapango ya asili ya Nubi curve.

Amesema  licha ya mkoa kuwa na vivutio vingi, sio rahisi kwa siku moja kuvimaliza vyote, kwahiyo hatua hiyo ni sehemu ya kufungua njia kwa wanakilimanjaro na watanzania wote, na hata wageni kutembelea vivutio mbalimbali vikiwemo vya asili vilivyopo maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro.

“Fikeni kujionea Ngoma za asili, vyakula na vinywaji vya asili kama Kirembwe, ugali wa ndizi, Ikatwe, ngararimu, ndizi choma za magadi, mbege, dengerua,kitalolo cha maziwa,kitawa,kiburu nk, wale, wanywe, lakini waone Ngoma za makabila ya asili ya wachaga, wapare na wamasai na mambo mengi mazuri”Amesema Mwenyekiti huyo wa KCF.