March 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jukwaa la Mchongoo ladhamiria kubadilisha soko la ajira

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Dar

KATIKA kukabiliana na tatizo la ajira kwa Vijana Jukwaa la Mtandao wa Utoaji wa Huduma, Nchini Tazania limelenga kuunganisha vijana wenye ujuzi vipaji na elimu mbalimbali na watoa huduma, na “Wanaotafuta huduma” kama njia ya kuweza kujikwamua kimaisha.

Hayo yameelezwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo, Julius Wambogo, amesema wanatumia teknolojia ya digitali ikiwa ni njia mpya ya kupata na kutoa huduma zinazosaidia kufanya kazi katika maisha ya kila siku.

Amesema katika kufanikisha hilo watu hao wataunganishwa na watoa huduma na wanaotafuta huduma na kujumuisha biashara zote, mashirika, na vyama katika ngazi za kitaifa, kikanda, na bara.

“Kila mwaka kampuni hufanya mambo tofauti ili kuongeza mauzo na shughuli zao, kusaka wajuzi na wataalam ila wanatumia nguvu nyingi na mitandao mingi sababu hakuna sehemu moja wanayopatikana na mara kwa mara wanatakiwa”amesema.

Ameeleza kuwa Mchongoo ni jukwaa linalowaunganisha watoa huduma mbalimbali hatua itakayotoa fursa mbalimbali.

“Mchongoo.com inakusudia kukusanya watoa huduma kuboresha utafutaji ili kutoa mahali ambapo kuna wenye ubunifu, wenye talanta na wenye uzoefu ambao wanaweza kuonyesha ujuzi wao na ili waweze kupatikana kwa urahisi.

“Pamoja na kuwa wazi kwa sasa tunapanga kuzindua rasmi mapema mwakani 2022, na itawagusa watu binafsi, makampuni, miradi ya shirika na ya viwandani, kwenye mtandao wa watoa huduma wenye ujuzi, wabunifu ambao wana utaalamu katika sekta mbalimbali katika nyanja za kazi ili kuungana na kufanya kazi kwa urahisi,”amesema Wambogo.

Amebainisha zaidi kuwa madhumuni mengine ni kubadilisha soko la kazi na utoaji wa huduma na kujenga tena kile kilichoathiriwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na Uviko-19.

“Mchongoo tunahitaji msaada wako na ushirika wako wasiliana nasi ili kujitolea au kuwekeza, hivyo kupitia teknolojia tumekusudia kubadilisha soko la ajira na utoaji huduma kwa kuboresha namana ya uapatikanaji, hii ni kutokana na athari mbalimbali zilizochangia kuyumba kwauchumi ikiwemo ugonjwa wa Corona,”amesema Wambogo.

Amesema kuwa katika Mchongoo ni huduma aina zote hutolewa kupitia jukwaa hilo la mtandaoni kwa kushirikiana na sekta binafsi, wizara na mataifa yenye dhumuni la kukuza uchumi wao na kuimarisha ubunifu pamoja na kuondoa umasikini katika jamii na kwamba mtandao huo ni muongozo.

Wambogo amesema kila mwaka zaidi ya wahitimu 1,000 humaliza masomo yao huku wengine zaidi ya 1,000 pia wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Pamoja na kwamba wanafunzi hao wanashindwa kuendelea na masomo makampuni mengi huingia sokoni kutafuta wataalamu mbalimbali kila mwaka baadhi ya makampuni bila mafanikio yakupata wanacho tafuta na kusahili,

Mkurugenzi wa jukwaa la Mchongoo Julius Wambogo

“Utafutaji huu huchukua muda na nguvu ya watendaji wa makampuni kwani uhitaji wa wataalamu unakuwa mkubwa,”amesema Wambogo.

Aidha amesema kuwa jukwaa la https://mchongoo.com itakuwa ni sehemu ya kutatua changamoto mbalimali za ajira kwa vijana na utafutaji ya watoa huduma wabunifu, wenye ujuzi na elimu wataonyesha ujuzi wao na kupatikana kwa urahisi kwaunganisha na watafuta huduma binafisi na makampuni yenye uhitaji.