
J
Na Mwandishi Wetu.
UONGOZI wa JKT Tanzania, ukiongozwa na baadhi ya viongozi wake pamoja na mchezaji Hassan Wahabi, umemtembelea kiungo wa Yanga SC, Pacôme Zouzoua, anayepatiwa matibabu baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Pacôme alipata jeraha wakati wa mechi kati ya Yanga na JKT Tanzania iliyochezwa Juni 30, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, na kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa matibabu.

Miongoni mwa waliofika kumjulia hali nyota huyo ni Afisa Habari wa JKT Tanzania, Masau Bwire, ambaye aliungana na ujumbe wa klabu hiyo kutoa pole na kumtakia nafuu ya haraka.
Hatua hiyo imepongezwa na wadau wa soka kama ishara ya mshikamano na utu ndani ya mchezo, huku wakimtakia Pacôme apone haraka na kurejea uwanjani kuendelea na majukumu yake.

More Stories
REA yaeleza utekelezaji wa Mikakati wa Nishati safi kwenye Tamasha la Kizimkazi 2026
JKCI yatakiwa kuendeleza kambi za Matibabu ya moyo nchini Comoro
Mwenge wazindua mradi wa maji, wanufaisha wananchi 34,000