May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akikata utepe kuzindua mradi wa maji katika chuo cha mafunzo ya awali RTS-Kihangaiko Picha na Luteni Selemani Semunyu

Jenerali Mabeyo afunda wanajeshi wapya JWTZ

Na Penina Malundo, TimesMajira Online

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo,amewataka askari wapya kuhakikisha wanalinda nchi kwa uadilifu kwani ndio jukumu lao kubwa na wanatakiwa kuishi ndani ya kiapo chao.

Pia amewataka kuhakikisha wanaishi na kiapo chao na kuwa tayari kutekeleza majukumu hayo mahala popote bila kuchagua kwani jeshi ndio linajua wapi wanaweza kutumika.

Aidha alikipongeza Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Kijeshi cha RTS Kihangaiko kutokana na usimamizi wa mafunzo na ujenzi wa miradi ya kujitegemea.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi zawadi mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mafunzo ya awali katika chuo cha mafunzo ya awali RTS-Kihangaiko Picha na Luteni Selemani Semunyu.

Jenerali Mabeyo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa sherehe za kuapa kwa Askari wapya kundi la 39 katika chuo hicho kilichopo Msata Bagamoyo Mkoani Pwani.

Amesema hana Shaka na mazoezi waliyopatiwa askari hao, kwani ameshuhudia kupitia vyombo vya habari pindi walipokuwa wakihitimisha mafunzo ya Porini.

Amesema kufanya zoezi la pamoja kwa kujumuisha vikosi mbalimbali tena kwa kutumia gharama za shule ni hatua kubwa ya kupongezwa. Ameongeza kuwa anafurahi kuona askari wapya mbele yake kwani ni ishara kwamba wameiva na wako imara katika kutumikia JWTZ .

“Pongezi kubwa ni kwa wakufunzi waliohakikisha wanafika hatua hiyo ya kuwafanya askari wetu wameiva kimazoezi na kuwa imara,”amesema

katika hatua nyingine aliwataka watu wote wenye jambo au masuala na jeshi hilo kutozunguka wafuate utaratibu wa kijeshi badala kutaka kuwatumia viongozi wengine wakati mkuu wa majeshi na wasaidizi wake wapo.amesema