May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Imani potofu ya tiba mionzi huchangia wagonjwa wengi wa saratani kufa

Na  Aveline  Kitomary,TimesMajira Online, Dar es Salaam.

SARATANI ni aina za ugonjwa unaotokana na seli za mwili zinazoanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na mwisho.

Miili yetu ina chembechembe  hai  nyingi ambazo huzaliana,hukua  na kufa kwa mpangilio maalum .

Chembechembe hizo zinapoharibika na kuanza kuzaliana  na kukua katika utaratibu usio wa kawaida  ndio husababisha saratani.

Chembechembe za saratani hufuata mfumo usio wa kawaida zinazaliana haraka zaidi  bila mpangilio na kukua  kwa haraka zaidi  na wakati mwingine kuwa na umbile kubwa zaidi.

Chembechembe hizo zisipothibitiwa  mapema zina uwezo wa kusambaa na kuota sehemu  nyingine ya mwili wa muhusika.

Ni uvimbe ambao unaweza kujitokeza mahali popote katika mwili wa binadamu ,uvimbe huo hauna maumivu yoyote mwanzoni.

Katika jamii kumekuwa na dhana mbalimbali kuwa endapo mtu atapata ugonjwa wa saratani uwezekano wa kupona haupo.

Pia wapo watu katika jamii ambao wanaamini kuwa ugonjwa huo unatokana na ushirikina hivyo hulazimika kutumia muda mwingi kwa waganga wa kienyeji.

Sio hilo tu kumekuwa na imani potofu kuhusu matibabu ya tiba mionzi kwa ugonjwa huo huku wengine wakiamini kuwa matibabu hayo hupelekea kifo.

Wakati wengine wakiwa na imani hizo wapo waliotumia tiba hiyo na wakafanikiwa kupona na maisha yao yakarejea kama awali.

Hali hii imeweza kumtokea Stella Herman(32) Mkazi wa Geita ambaye anasimuli jinsi jamii ilivyokuwa inamkatisha tamaa baada ya kupata ugonjwa saratani.

Stella ni Mzaliwa wa Wilaya ya Babati ,Mkoani Manyara lakini kwa sasa makazi yake yapo Mkoa wa Geita kutokana na shughuli anayofanya.

Ni mwalimu wa shule ya sekondari  Ruzewe  Bukombe ambaye anafundisha somo la Kiingereza.

Ni kawaida yake kila asubuhi siku ya kazi kuamka na kujiandaa kwenda katika jukumu la kujenga nchi kama ilivyo kwa vijana wengine.

Awali afya ilikuwa njema kabisa na aliweza kuendelea na majukumu japokuwa alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Tatizo hilo halikumsumbua kutokana na kutumia dawa mara kwa mara.

Lakini ni siku moja tu ilikuja tofauti kwa Stella mara baada ya kuona mabadiliko kwenye kinyesi chake.

Mwanzo kilikuwa cha kawaida lakini sasa kinaonekana kuwa na damu.

“Ilikuwa sio kitu cha kawaida kabisa kwangu nilihisi kuna tatizo mwanzo wakati mwingine nilifikiri ni vidonda vya tunambo vinasababisha hali hiyo lakini sikuliaminia sana hilo,”anasimulia Stella.

Anasema tatizo la kuona haja kubwa yenye damu ilianza mwaka 2019 hata hivyo alipoenda mmoja wapo ya hospitali aliambiwa tatizo ni vidonda vya tumbo.

“Lakini bado nilikuwa na maswali mbona vidonda vya tumbo nimekuwa navyo muda mrefu tangu 2011 na sijawahi kupata haja kubwa yenye damu?,”anahoji.

“Nilipewa dawa nikaenda kutumia lakini hakuna kilichobadilika hali ilizidi kuwa ile ile, Madakatari hawakuwa na ufahamu wowote hospitali za Wilaya na Mkoa kuhusu tatizo lililokuwa linanisibua  wanachelewa kugundu hadi dalili zikue.

“Nilifanikiwa kufika hospitalini haraka  baada ya kutokuridhishwa niliomba ruhusa kwa mkuu wa shule akanizungusha nikaamua kwenda halmashauri nikapata kibali baada ya hapo nilienda hospitali Mwanza,”anaeleza.

Stella anasema alipimwa akakutwa na uvimbe kwenye utumbo  hata hivyo hawakuweza kutoa nyama ya kwenda kupima.

“Ni kwasababu uvimbe ulikuwa na sehemu kwenye sehemu,Kaka yangu alinishauri niende Muhimbili.

“Ila wakati nafikiria hilo niliona clip  moja ya Daktari Bingwa wa Saratani akiongea ambayo ilikuwa kwenye group akihojiwa na Tv,akataja dalili za kwanza za satania ya utumbu mpana kuwa ni choo chenye damu bila maumivi na mimi nilikuwa siumwi.

“Nikaenda Muhimbili nilivyofika nikafanyiwa kipimo cha Mwanza wakatoa majibu  wakafanikiwa kutoa kinyama wakakuta niko stage 2.

Stella baada ya matibabu na kupona

APATA  MATIBABU

Stella anaeleza kuwa alivyofika na kufanyiwa vipimo kadhaa akaanza wakagundua kuwa alikuwa na saratani ya utumbu mpana na akaanza kupata matibabu.

“Nikafanyiwa vipimo vya MRI,CT- SCAN ,Ultrasound,X- Ray na damu  baada ya hapo walijua ugonjwa ulisambaa kwa kiasi gani.

“Nilifanyiwa upasuaji upasuaji ambao ulikuwa wa kuondoa sehemu yenye uvimbe nilikuwa napata choo sehemu ya haja kubwa na ndogo nikapata fistula ambapo ilibidi nifanyiwe upasuaji mwingine Aprili 30,2020 ambao ni wakuweka nafasi ya haja kubwa.

UTHUBUTU WA TIBA MIONZI

Hii ilikuwa hatua ya kuogopesha zaidi kwa Stella kutoka ana kusikia habari mbaya kuhusu tiba mionzi kutoka kwa watu mbalimbali.

Anasema alijitoa kufa ilia aweze kupata aina hiyo ya matibabu.

Hapa anaeleza “Nilipata matibabu ya mionzi ocean road niliamini kuwa kifo ni cha Mungu na nilisoma mambo mengi kuhusu mionzi nikajipa imani.

“Wasiwasi unakuja pale watu wanavyosema tiba mionzi inaua nikasema kama nitakufa ni mipango ya  Mungu nikasema matibabu ya saratani yote nitafanya.

“ Nilikutana na watu wengi pale ocean road wanasema hawataki kufanyiwa mionzi wanaongopa wanasema huwa inaua kwasababu mionzi inaua seli za kansa hivyo inaongeza siku niliamini mionzi inaenda kuniongezea siku  japo nilijiuliza maswali mengi mwisho nikaamua.

Anasema watu wengi wanaogopa mionzi kwasababu wanaenda wakiwa na hatua ya juu ya saratani hivyo wakipata matibabu hali inakuwa mbaya na kufanya kupoteza maisha.

“Mionzi sio hatari tunaongeza mionzi tatizo ni watu kuchelewa halafu  hawana imani na tiba.

BAADA YA MATIBABU

Stella nasema baada ya kupata matibabu hali yake imeimarika na sasa anaendelea na kazi yake ya kufundisha wanafunzi akiwa mwenye furaha na matumaini ya kuosonga mbele.

“Sasa hivi naendelea vizuri nimepona naendelea na kazi nimeanza kuingia darasani kufundisha nitaendelea kuhudhuria kliniki ili niweze kupona kabisa.

ANAKEMEA  IMANI POTOFU

Anasema zipo imani potofu katika jamii kuwa ugonjwa wa saratani ni uchawi na pia wanadai matibabu ya mionzi yanaua kitu ambacho sio sahihi.

“sifurahishwi hata kidogo na imani potofu cha muhimu mtu akiona anadalili ambayo sio nzuri afanye jitihada za kutafuta tatizo ni nini? tuwe na tabia ya kuchekia afya zetu mara kwa mara itasaidia.

“Tiba mionzi haiui  inaongeza maisha inaponya jamii iachane na imani kuwa tiba mionzi inaua kama mtu akienda hospitali ndogo ikaonekana hana ugonjwa ni bora akapate matibabu makubwa wasiseme wamelogwa.

“Kinachonisikitisha zaidi  wagonjwa niliozungumza nao Ocean Road wengi wamepitia kwa waganga.

“wagonjwa wa saratani wanakufa kwasababu msongo ya mawazo watu wanasema hutapona unakufa hivyo wanafikiri ukishapata saratani ndio basi ,wagonjwa wote wameshawahi ambiwa kuwa hawawezi kupona ni kufa tu lakini saratani inatibika,”anaongea Stella.

Anaiomba serikali kutoa baadhi ya vifaa vya upimaji kwa saratani za ain mbalimbali.

“ Tukienda tunapimwa shingo ya kizazi na matiti lakini kuna saratani zingine , serikali ilitoe elimu zaidi kila sehemu ya nchi jamii yote ya chini ijue saratani inapona.

“Serikali isaidie watu wanajitolea kutoa elimu ya saratani na pia ni muhimu wahudumu wa afya kupata elimu ili wasicheleweshe wagonjwa.

“wapo madaktari Waliniambia kuwa ingekuwa kansa ungewa umekonda angalia ulivyokuwa na afya nzuri hawakuweza kunipa kibali chakutibiwa hospitali kubwa.

NINATO ELIMU KWA MADAKTARI

“Nimepanga kuenda kuwapa madaktari elimu niwaambie dalili za saratani zikoje ni tawaelimisha hivyo nitafurahi binafsi ili waweze kuwasaidia watu wengine

“Serili watoe elimu kwa wahudumu wa afya hadi madaktari wa vijijini.

“Hata kwa daktari ngazi ya cheti wapewe elimu ya saratani hata nesi apewe elimu wote kuanzia ngazi za chini hadi juu wapate elimu ili rufaa ipatikana na saratani itibike katika hatua ya mwanzo.

UFAHAMU KUHUSU TIBA MIONZI

Utafiti  uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) umeonyesha kuwa asilimia 72 ya wananchi hawana uelewa kuhusu vipimo na tiba ya mionzi huku asilimia 64 ya wagonjwa wakipata huduma hiyo kwa kuwaamini madaktari.

Mtaalamu bingwa wa matumizi ya mionzi katika taasisi hiyo, Steven Mkoloma,anasema  hali ya hofu huweza kufanya wagonjwa wakaogopa kufika hospitali kupata matibabu ya mionzi.

Mkoloma anasema hali hiyo ya uelewa mdogo inaweza kusababisha wagonjwa kuchelewa kutibiwa na hata wengine kupoteza maisha kwa kuhofia matibabu hayo.

Utafiti huo uliofanyika katika mikoa mitano nchini ukihusisha watu 30 kwa kila mkoa, pia ulibaini asilimia 54 ya madaktari wa ngazi zote walikuwa na ufahamu kuhusu vipimo na tiba mionzi.

“Huu ni utafiti ambao ulikuwa unaangalia ufahamu na uelewa wa jamii kuhusu mionzi inayotumika katika uchunguzi  wa magonjwa na tiba kwa Tanzania, utafiti huu ulifanyika katika mikoa mitano tofauti ukiuliza swali moja, na mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Kilimajaro, Mwanza, Mbeya na Ruvuma.

“Katika kila mkoa kulikuwa na washiriki 30 ikiwa 10 ni wagonjwa ambao waliandikiwa kufanya vipimo vya X-ray au matibabu yanayohusisha mionzi, 10 madaktari na 10 wananchi ambao hawajawahi kuandikiwa kufanya vipimo vinavyohusiana na mionzi.

“Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kwamba asilimia 72 ya watu ambao hawakuandikiwa vipimo hivyo walikuwa na ufahamu mdogo wa mambo ya mionzi, asilimia 64 ya wagonjwa walikuwa na ufahamu mdogo, lakini asilimia 54 tu ya madaktari katika ngazi zote kuanzia ‘clinical officer’ na ‘specialist’ walikuwa na ufahamu wa mambo ya mionzi.

“Lakini pamoja na kwamba hawa wagonjwa na raia ambao hawajaandikiwa vipimo vya miozi ufahamu wao ulikuwa mdogo, lakini walikuwa na ujasiri wa kuendelea kupata huduma za mionzi huku kigezo kikubwa ambacho walikitazama ni imani yao kwa daktari,” anafafanua  mtafiti huyo.

Anasema majumuisho ya utafiti huo yanaonyesha ufahamu mzima wa mambo ya miozi kwa Watanzania uko chini.

Anaeleza kuwa sababu za asilimia 54 ya madaktari kuwa na uelewa ni baada ya kupata mafunzo shuleni.

“Hali hiyo inajulisha kuwa kuna haja ya elimu kutolewa zaidi hata kwa wahudumu wa afya.

“Kazi inatakiwa kufanyika kwa sababu kama hawa asilimia 72 hali ni hiyo, na ambao wamekwenda kufanya huduma kwa sababu wana imani na daktari na wakakutana na daktari ambaye hana ufahamu, ni rahisi kuahirisha huduma kwa sababu ya kukosa taarifa sahihi.

“Tunashauri Serikali na mamlaka zinazohusika na taarifa kwa jamii kuweka utaratibu ambao wahudumu wa afya wa kada mbalimbali pamoja na wananchi wataweza kupata taarifa za kutosha,” anasema Mkoloma.

Anasema uchunguzi wa saratani  unahusisha sana mionzi, lakini matibabu inategemea mionzi, kwa hivyo kama mgonjwa au jamii watakuwa na taarifa sahihi, wanaweza kupata watu wengi wa kupata vipimo au matibabu na hivyo kupunguza kiwango cha wagonjwa wanaochelewa kufika hospitali au kupoteza maisha kabla hawajafika.

“Kimsingi watu wanaogopa kwa sababu wanaamini mionzi inaua seli, lakini kisayansi hutibu kwa sababu eneo linalofikiwa na mionzi ni lile tu ambalo lina tatizo, tunaua zile seli na kuruhusu mwili kutengeneza seli mpya ambazo hazina ugonjwa,” anasema Mkoloma.

TIBA MIONZI NI SALAMA

Daktari Bingwa wa Ugonjwa wa Saratani wa Taasisi ya Tiba ya Saratani Ocean Road (ORCI), Hellen Makwani aliiambia Jarida la Majira ya Afya  kuwa tiba mionzi ni salama na yenye kuminika zaidi kwa wagonjwa wa saratani.

“Napenda kuwaambia kuwa wasiogope tiba mionzi  ni tiba salama na yenye kuvumilika hasa kwa teknolojia ya kisasa ya mashine za kisasa aina ya LINEAR accelerator ambayo husaidia kutibu kwa kiwango cha juu.

“Pia tiba hii inatumia Dunia nzima na imethibitika kuwa salama na yenye matokeo mazuri ,elimu zidi inatakiwa ili jamii iondoe hofu pamoja na imani potofu juu ya tiba mionzi,”anashauri Dk Makwani.