June 30, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ilemela yaendelea kupata hati safi

Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2024/2025 baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu za Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza halmshauri hiyo ilipata hati safi.

Hayo yamebainishwa Juni 29,2026 na Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoa wa Mwanza CPA. Richson Ringo,wakati akiwasilisha taarifa fupi ya matokeo ya ukaguzi wa hoja za CAG kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

CPA.Ringo amesema, kuwa kwa kipindi cha miaka minne (4) mfululizo yaani kuanzia mwaka 2021/2022, 2022/2023 na 2023/2024 na 2024/2025 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imeendelea kupata hati safi. 

Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa (Local Government Finance Act, 1982), iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, kila baada ya mwaka wa fedha kuisha halmashauri zinapaswa kuwasilisha taarifa zake za hesabu kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ajili ya ukaguzi.

Hata hivyo baada ya kufanyiwa ukaguzi, halmashauri hupewa nafasi ya kujibu hoja zake.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuendelea kupata hati inayoridhisha kwa miaka minne mfululizo.

Ambapo amesema kuwa Ilemela ni miongoni mwa halmashauri mkoani Mwanza inayofanya vizuri katika suala la ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa takwimu kwani mapato yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka na hivyo kuitaka kutumia mapato hayo kwa utekelezaji wa miradi mikubwa.

    Â