Na Penina Malundo, TimesMajira Online
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, ametangaza kifo cha Naibu Kamishna wa Polisi, Dhahiri Kidavashari kilichotokea leo katika Hospitali ya Christian Medical Center Trust (DCMCT) iliyopo, Dodoma ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya IGP Sirro, Kamanda Dhahiri Kidavashari, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Novemba, 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Aidha IGP Sirro, amesema kuwa msiba upo Kisasa,Nyumba mia tatu jijini hapo huku taratibu za mazishi zikiwa zinaendelea.
More Stories
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais
NIDA yawakumbusha wananchi kuchukua vitambulisho vyao