December 6, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Idris Sultan: Sivai tena nguo hizi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa vichekesho hapa nchini, Idris Sultan amesema nguo alizozivaa siku ambayo kesi yake inafutwa hatovaa tena.

Akiongelea hilo kupitia Ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ametupia picha aliyovaa nguo zenye rangi nyekundu Idris amesema nguo hizo zina historia za matashtiti.

“Hizi nguo nadhani ndio mara ya mwisho kuzivaa. Zina historia za matashtiti tu kwakweli. Siku ya kwanza kufunguliwa kesi nilikuwa nimezivaa halafu siku nafutiwa kesi zangu nikawa nimezivaa. Naomba serikali izipige marufuku hizi nguo kuuzwa na kuvaliwa kote nchini,” amesema Idris.