April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, marehemu Isihaka Sengo

Hatimaye Naibu Meya Morogoro azikwa na watu wasiozidi 10

Na Severin Blasio, Morogoro

MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Lowata Ole Sanare amesema mazishi ya Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Isihaka Sengo, ambayo yamefanyika  jana saa 10  yamehudhuriwa n watu wasiozidi 10.

Utaratibu wa mazishi ya Naibu Meya Sengo uliwekwa wazi jana na RC Ole Sanare alipokutana na Kamati ya Ulinzi na Usala Mkoa wa Morogoro na waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa ufafanua wa mazishi hayo.

Amesema mazishi yake yatafanyika nyumbani kwa asili kwa naibu meya huyo eneo la Kibwe na kwamba yatasimamiwa na Serikali.

“Hakuna sababu ya kusubiri majibu ya kitabibu kutoka Dar es Salaam, mwili utazikwa leo (jana Aprili 28,2020)  kwani tayari muongozo ulishatolewa kuwa hakuna mikusanyiko, hivyo ni vyema mwili huo ukazikwa bila kusubiri majibu hayo,”alifafanua Ole Sanare.

Amesema jana (juzi) Serikali ilizuia mazishi hayo yasifanyike hadi sampuli zitakapotoa majibu ya sababu za kifo chake baada ya kuwepo utata  dhidi ya kifo hicho.

“Lakini hadi sasa (jana) mchana hapakuwa na lolote hivyo Serikali inaamua kutoa maelekezo hayo na yatafanyika kwa usimamizi wa Serikali,” amesema.

Naibu Meya Sengo aliyezaliwa mwaka 1961 alikuwa diwani wa kata  ya Kiwanja cha Ndege mjini humo akishika wadhifa huo baada kurithi kiti hicho kutoka kwa aliyekuwa diwani wa kata hiyo, God Mkondya mwaka 2018.

Utata wa kifo chake ulijitokeza baada ya Mganga Mkuu Manispaa ya Morogoro, Ikaji Rashid kufika nyumbani kwa marehemu mchana na kuwakuta ndugu na jamaa wakijindaa kwenda kuzika.

Baada ya hapo aliwataka kusitisha mazishi na mwili wake upelekwe mochuari kwa uchunguzi. Mganga huyo alisema baada ya ofisi yake kupata ataarifa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa kwa mara ya mwisho kuna viashiria vya marehemu kuwa na maabukizi ya Corona.

“Serikali inasitisha mazishi yake hadi itakapotangazwa vinginevyo na mwili unakwenda kuhifadhiwa chumba cha maiti tutachukua sampuli na kuzituma Dar es Salaam kwa uchunguzi,”alisema Dkt. Rashid.

Huyo ni mtu wa tatu mazishi yake kutangazwa kusimamiwa na Serikali na kuhudhuriwa na watu wasiozidi 10.

Mtu wa kwanza mazishi yake kuhudhuria na watu wasiozidi 10 alikuwa Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Getrude Rwakatare, aliyezikwa hivi karibuni Mikocheni jijini Dar es Salaam, huku jana pia mazishi ya DC wa Mtwara, Evod Mmanda akizikwa na Serikali na mazishi yake kuhudhuriwa na watu wasiozidi 10.