May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hatifungani ya Twiga yaorodheshwa katika soko la Hisa

Na Mwandishi wetu,Timesmajira Online

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) hii leo tumeorodhesha hati fungani yetu ya kwanza kabisa ya NBC Twiga katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), huku Serikali ikitupongeza kwa namna tunavyoandaa mfumo jumuishi wa kifedha hapa nchini.

Hati fungani hiyo ya muda wa kati ya TZS 300 bilioni, ilifunguliwa katika soko la awali tarehe 31 Oktoba 2022, na hivi karibuni Benki ya NBC tulitangaza kufunga mauzo ya hati fungani hiyo kwa mafanikio makubwa baada ya kukusanya kiasi cha sh Bil 38.9 ikilinganishwa na sh bil 30 zilizotarajiwa kukusanywa hapo awali. Mafanikio hayo ni asilimia 130 ya malengo yaliyotarajiwa..

Kupitia hati fungani hiyo, tunalenga kukusanya kiasi cha Sh 300 Bilioni ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, Kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuorodhesha NBC Twiga Bond kwenye soko la Hisa la Dar es Salaam iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Japhet Justine aliipongeza Benki ya NBC kwa hatua hiyo kwa kuwa itafungua zaidi soko la hisa huku pia akibainisha kuwa upatokanaji wa fedha hizo hizo utasaidia zaidi jamii ya wafanyabiashara nchini.

‘Mbali na kuunga mkono msukumo wa ujumuishi wa kifedha kupitia hati fungani hii, serikali inafurahishwa zaidi kujua kwamba faida za hati funganii hii inakwenda mbali zaidi kwa kugusa mnyororo mzima wa wadau wa kilimo na wajasariamali. Serikali inapongeza benki ya NBC kwa ubunifu huu,’’ alisema.

Nae Mtendaji kuu wa Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana Nicodemus Mkama, licha ya kuipongeza Benki ya NBC kwa hatua hiyo kubwa., amesema Fedha zilizopatikana kupitia mauzo ya hatifungani ya Twiga zitatumika kugharamia shughuli za maendeleo ya benki ya NBC, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa kampuni ndogo na za kati za ujasiriamali (Small and Medium Enterprises – SMEs); mikopo kwa wawekezaji wadogo wadogo (Retail Investors) yenye lengo la kukuza na kuendeleza ujasiriamali hapa nchini; mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo; mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara zinazosimamiwa na zinazofaidisha akina mama na vijana; Hatua hii ni muhimu, kwani inatarajiwa kuwa na matokeo chanya