
Na Mwandishi Wetu
NCHI waandaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) wamesaini hati ya makubaliano ya pamoja inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027 tarehe 11 Mei, 2026.
Nchi hizo ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda zimesaini hati hiyo kwa lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.
Utiaji saini makubaliano hayo yameshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motssepe.
Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais Wallace Karia.

More Stories
Kikundi cha Mshikemshike cha badilisha maisha kwa Ufugaji wa Kondoo Shinyanga
NMB yaibuka Superbrand Afrika Mashariki 2026-2028
MNH Mloganzila yaanza kambi ya Upasuaji wa Nyonga,Magoti na Mabega