November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

GSM yatenga milioni 50 kununua vifaa vya barabara

Na Penina Malundo,Timesmajira,Online

KAMPUNI ya Ghalib Said Mohamed (GSM) imetenga kiasi cha Sh miloni 50 kwaajili ya kununua  vifaa vya barabarani kulingana na changamoto za sehemu hizo ikiwa ni hatua za kuunga mkono serikali juhudi za kupambana na ajali za  barabarani.

Akizungumza jana wakati akitoa Vizibao “reflector jacket” 100  kwa Wilaya ya Temeke, Afisa masoko na mawasiliano Smart  Deus, alisema   kama wadau wa usafirishaji kupitia kampuni yao  ya Galco  ya usafirishaji wa mizigo na bidhaa mbalimbali katika sekta ya usafirishaji   ambazo zitaweza kutumika na jeshi la polisi  kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabara katika Wilaya ya Temeke.

“Progamu hii ni endelevu sisi kama GSM kupitia kampuni yetu ya usafirishaji  hii ni kitu endelevu ambayo sasa tumeanza na wilaya ya Temeke na mradi huu utakuwa ni kama wenye gharama millioni 50 za kitanzania, amabayo tukitoka wilaya ya temeke tutaenda mkoa na mkoa kuenda kuangalia changamoto gani ambazo zipo,”Amesema Deus  

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Ya Temeke, Katibu tawala wa Wilaya hiyo Bupe Mwakibite ametoa  shukrani na  hongera kwa Gsm kwa hatua ya  kuunga Mkono suala la usalama barabarani.

“ Hii ni hasa  kuhakikisha usalama barabarani kwa wananchi na kunga mkono jitahada ya Rais Samia Suluhu Hassan  kuwa wananchi wa wilaya ya Temeke na Tanzania inabaki kuwa salama hasa kwa kuzingatia usalama barabarani na susaidia jeshi la polisi kufanya kazi katika ufanisi mkubwa” Alisema Bupe

Kwa upande wake SP Africanus Sulle amesema Reflekta  zitasaidia kuonekana kwa askari pale mwanga unakuwa mdogo, wakati wa jioni, yakati kunakuwa na wingu au vumbi kuzingatia barabara ya Kilwa ambayo inaendelea na ujenzi ili saidia madereva kuwaona askari kwajili ya kuzingatia usalama na uratibu wa muelekeo.

“Nitaendelea kuwaomba GSM kama kampuni ambao ni wadau wetu wakubwa sana waendelee kutusaidia,  bado tunahitaji tochi ile ya kuongozea magari, Askari pamoja anareflector lakini anaongoza gari kwa mikono tunazo tochi kwa sababu ni wadau watuongezee tochi ili tuendelee kufanya kazi yetu ya barabarani na Wilya yetu ya temeke iendelee kuwa vizuri.”amesema

Aidha Sulle amesema wilaya ya Temeke ipo salama kwa ajali, kwasababu ya juhudi ya wadau kutoa vifaa na pia wapinganaji wamejipanga vizuri na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, shule za kandokando ya barabara, bodaboda.