Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
TAMASHA la FinTech kuibua uwezo wa FinTech nchini na kuonyesha fursa kwa wawekezaji wa kimataifa kujitosa katika soko la Tanzania ili kuimarisha zaidi mfumo wa teknolojia na ushirikiano kati ya Tanzania na Global FinTech.
Akizungumzia wakati wa Ufunguzi wa Tamasha hilo Leo Novemba 08, 2023 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Eastern Star Group Deogratius John Kilawe amesema tukio hili ni mawazo na teknolojia mpya iliyojaa midahalo na ushirikiano wenye tija, na mitandao isiyo na kikomo ambayo inahusisha akili kubwa zaidi kutoka kwa ulimwengu wa Fedha na Teknolojia.
Aliongeza kuwa, Tamasha la FINTECH lilianza Mwaka 2016, ambapo Katika Tamasha lililopita liliweka maazimio mbalimbali ambayo tathmini na kutekeleza maazimio hayo na mikakati kwa ajili ya kutekeleza yale ambayo yameshindwa kukamilisha katika kipindi cha nyuma.
Tamasha hilo litatoa fursa kwa wadau wote wa FINTECH kukutana kwa pamoja na kutathmini utekelezaji katika hatua zote ili kuweza kupiga hatua katika kufanikisha hilo.
“Mafanikio ya kuwezesha financial inclusion process kuwa rahisi, financial retrace kuwezesha Tanzania kuwa mstari wa mbele na kukuza Teknolojia ya FINTECH”.
Aidha, Tamasha hilo litawaleta pamoja Afrika Mashariki na kubadilishana ujuzi wa kimataifa kutoka kwa wasomi wakuu, watendaji, na viongozi katika vipindi vilivyofikiriwa upya vinavyohusu kubuni, kujenga na kuhakikisha huduma endelevu za kifedha kwa Wavuti.
Hivyo, FINTECH FESTIVAL ndilo tukio kubwa zaidi la Teknolojia ya Kifedha katika Afrika Mashariki, likitoa jukwaa kwa jumuiya ya FinTech kuungana, kushirikiana kwa pamoja, Ikiwa wewe ni mwanzilishi wa kampuni ya teknolojia, mwekezaji, taasisi ya fedha, taasisi ya utafiti, au mtaalamu wa uvumbuzi, utakuwa na jukumu muhimu katika kuimarisha zaidi mfumo wa Teknolojia na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Global FinTech.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua