May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ewura kuthibiti uuzaji holela mafuta kwenye chupa vijijini

Na  Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya

MAMLAKA ya  udhibiti wa nishati ya mafuta nchin(EWURA)imesema kuwa ili kuondoa biashara za uuzwaji holela wa mafuta kwenye chupa unaofanywa maeneo ya vijijini kuwezesha kampuni zenye uwezo kujenga vituo vya gharama nafuu vijijini  ili kufikisha huduma bora.

Hayo yamesemwa jana na Meneja wa Mawasiliano na uhusiano Ewura Makao Makuu, Titus Kaguo wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari mikoa ya Nyanda za Juu Kusini namna ya kuandika habari zinazohusina na Mamlaka hiyo.

Alisema kuwa lengo ni kuboresha upatikanaji wa huduma hizo si mijini peke bali hata viijijini sambamba na kuendelea kukabiliana na udhibiti wa nishati ya maji,gesi na mafuta kwa kuhakikisha vinakuwa na ubora kwa matumizi ya wateja na wananchi kwa ujumla”amesema .

 Hata hivyo , amewataka wamiliki wa magari ya umma na binafsi kutoa taarifa za wafanyabishara wa vituo vya mafuta wanaotumia ujanja kuwaibia kwa kuchakachua pampu za kujazia mafuta ambao umeibuka katika baadhi ya maeneo nchini.

 “Kuna mchezo ambao unaweka mafuta lita 10, lakini kwa namna wanavyofanya kwenye pampu ukapata lita 5 sasa ili kuwabaini naomba muwe mnashuka na kushuhudia mashine zinavyosima sambamba na kuchukua risiti ambazo zitatusaidia ushahidi kama Mamlaka yenye dhamana,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Ewura, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Karim Ally amesema kuwa ili kudhibiti mchezo huo kuna kila sababu wanachi kusaidiana na Ewura kutoa taarifa zinazohusiana na Sekta wanazosimamia.

 Akizungumzia mafunzo hayo, mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha TBC Mkoa wa Katavi, Hosea Cheyo alitolea mfano, akisema amenunua mafuta ya Sh30,000 kwenye moja mkoani humo Oktoba 8, 2021 na kuambulia lita saba tu, akiomba Ewura ifuatilie suala hilo.

“Tunaomba Ewura mfuatilie hili suala halina afya kabisa kwa wateja mimi hapa leo narudi pale niliponunua mafuta  kudai haki yangu ,unaweza ukute wengi wanatendwa kwenye vituo vya mafuta tunaomba Ewura mlione hili “amesema Cheyo.