Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Butiama
Mgombea mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi ametembelea familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,kijiji cha Mwitongo, Wilaya ya Butiama.mkoano Mara.
Akiwa nyumbani kwa familia hiyo Dkt.Nchimbi amepata wasaha wa kuzuru kaburi la Mwalimu Nyerere na kuweka shada la maua, kuwasha mishumaa pamoja na kumwombea.
Dkt.Nchimbi ametembelea familia hiyo Agosti 30, 2025 ikiwa ni siku ya kwanza kuingia mkoani Mara kwa ajili ya kufanya kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025.

More Stories
OUT Yaweka Ubunifu Msingi wa Elimu Huria Mtandaoni
Nmb yaunga mkono afya ya Watumishi kupitia Shimisemita
Ushetu yatoa zabuni za sh.90.48 kwa makundi Maalum