LONDON, England
NYOTA nambari moja ulimwenguni katika mchezo wa tenis
kwa upande wa wanaume Novak Djokovic, amefanikiwa
kunyakuwa ubingwa wa tenis katika mashndano ya Wimbledon
kwenye mchezo wa fainali uliofanyika mwishoni mwa wiki
nchini Uingereza.
Djokovic, mwenye umri wa miaka 34 raia wa Serbia ameweka
rekodi ya Grand Slam ya 20 kwa kuibuka na ushindi wa
seti 6-7 (4/7), 6-4, 6-4, 6-3 dhidi ya slugger Matteo
Berrettin raia wa Italia.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Djokovic
amesema,amefurahi sana kunyakuwa taji la Wimbledon huku
ikiwa Grand Slam yake ya 20, kwani alicheza sana vizuri
katika fainali hiyo.
Djokovic,
ambaye alikuwa akicheza fainali yake ya 30
kwenye Slams, aliongeza
bada ya kunyakuwa Australia
Open, Roland Garros
na na US Open.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania