May 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Halima Bulembo apongeza kiasi cha asilimia 23.3 ya mishahara

Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online, Tanga

Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wamesema asilimia 23.3 ilioongezwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mishahara yao itawapa unafuu kwenye maisha na hivyo kumaliza kilio chao cha muda mrefu.

Ongezeko la mishahara la asilimia 23.3 kuwa imelenga kuongeza ufanisi wa kazi,kujituma na kupunguza makali ya maisha.

Akiongea na waandishi wa habari Kwa niaba ya watumishi wa wilaya hiyo Mkuu wa wilaya hiyo Halima Bulembo amesema kuwa wamepata faraja Kwa uamuzi huo na hivyo kuongeza Imani Kwa serikali Yao Kwani kilikuwa ni kilio Chao Cha muda mrefu.

Bulembo amesema wafanyakazi wengi wamepata faraja baada ya tamko la mheshimiwa Rais na wameongeza imani na serikali yao.

“Kwa niaba ya watumishi wa Muheza tunamuombea Rais Mungu amjaalie uzima aweze kuendelea kutuongoza watanzania na kutujali Katika nyanja zote na tuahidi kuendelea kuwa na imani Nae “amesema DC Bulembo.

Mmoja wa watumishi hao Saumu Mohamed amesema wanamshukuru Rais Kwa ongezeko Hilo kwani watumishi wamefurahi Sana na kumuombea Kwa Mungu aweze kuleta mabadiliko mengi ndani ya nchi hii.

Kwa upande wake Afisa Elimu Selapyone Bashangwe amempongeza Rais Kwa uamuzi wake wa kuongeza mshahara kwani umekuja wakati mwafakaOngezeko la mishahara limekuwa likipigiwa kelele na wafanyakazi kwa muda mrefu hasa wakati wa sherehe za wafanyakazi wakitaka serikali kuongeza kiwango cha mshahara ili kiendane na maisha halisi yaliyopo.