Na Hadija Bagasha,Iringa
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema endapo kitapata ridhaa ya kuongoza nchi kitawekeza kwenye rasilimali watu ikiwemo afya na elimu.
Hayo yalisemwa na mgombea urais Prof. Ibrahimu Lipumba kupitia chama hicho wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo alisema kama watu hawana elimu na afya bora ukiwekeza kwenye vitu haitawasaidia chochote.
Lipumba alisema Serikali ya CCM imekuwa ikiwekeza kwenye kununua vitu kama vile ndege badala ya kuwekeza kwenye miundombinu muhimu ya afya na elimu.
‘Endapo tutapewa ridhaa Sera ya CUF itawekeza kwenye vitu muhimu vya afya na elimu ili viweze kuja kuwasaidia watanzania katika kujikwamua na umaskini.,”
Kama Taifa lazima tuwe na utaratibu wa kuhakikisha watoto wanapata lishe bora ili kujikengea kinga ya mwili na Serikali ina kila sababu ya kuhakikisha wanapata elimu bora.
Profesa Lipumba alisema muungano ni muhimu na endapo watachaguliwa wataimarisha muungano kati ya Tanzania bara na Zanzibar na kuwa na haki sawa kwa pande zote mbili.
Alisema watakapopata ridhaa hiyo ya kuongoza nchi wataendeleza muungano kwa kuwa ni muhimu kwa Taifa letu.
Katika hatua nyingine mgombea urais huyo alisema Serikali ya CCM imeiacha solemba sekta ya kilimo na bila mapinduzi ya kilimo hawawezi kuleta mapinduzi ya viwanda hivyo CUF inahitaji kuleta mabadiliko na mapinduzi katika sekta hiyo.
Alisema wanahitaji kuleta mabadiliko ili pawepo na mzunguko wa fedha kwani wananchi wa Kilolo ni watu wanaojishughulisha na kilimo lakini hawana msaada wowote wowote wanaoupata kutoka serikalini.
Tunaomba kura zenu ili biashara zitoke na wananchi waweze kufanya biashara uwekezaji uongezeke vitunguu vipate soko sio tu Tanzania mpaka Africa mashariki yote watu wapewe utaalamu wa kuweza kuongeza tija katika shuhjuli zao za kilimo…wapate zana na kuweza kumwagilia na za kilimo.
Hata hivyo alisema kuwa unapoongeza tija kwenye kilimo ndipo unapopata uwezo wa kuendeleza viwanda kwani kilimo kinatoa chakula na endapo kilimo kikiwa na tija uzalishaji utaongezeka.
Kwa upande wake mgombea mwenza Hamida Abdalah Huweishi amewataka vijana wasijutie kuzaliwa kwani muda uliopita siyo muafaka kwani cuf itawaboresha katika kila aina ya sekta kwa kutumia rasilimali za nchi zilizopo.
Vijana siyo taifa la kesho ni Taifa la leo Sera ya Taifa la kesho ipo CCM na imewaweka kwenye uongo mtupu na kuacha rushwa itawale pigeni kura CUF ili muyaone mabadaliko hamkuzaliwa kuja kuongeza idadi ya makaburi CUF imedhamiria kuwainua,’alisema Mgombea.
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8