December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkurugenzi wa Uchaguzi CHADEMA, Reggy Munisi (kulia) akimkabidhi fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Wakala wa Tundu Lissu, David Jumbe, leo katika Makao Makuu ya CHADEMA, Kinondoni, Dar es Salaam.

Chadema kumekucha utoaji wa fomu Urais,Ubunge na Uwakilishi, Tundu Lissu achukuliwa fomu

Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Dar es Salaam

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ), kimeanza rasmi ratiba ya shughuli ya uchukuaji, kutafuta wadhamini na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , Urais wa Zanzibar, Ubunge wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania na Uwakilishi wa Baraza la wawakilishi Zanzibar leo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CHADEMA Reggy Munisi amemkabidhi fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi ya Rais kuptia chama hicho wakala wa Tundu Lissu David Jumbe (hayupo pichani)leo mapema.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo imesema watia nia nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watachukua fomu zao za kugombea Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Imesema kwa watia nia wa Urais wa Zanzibar, watachukua fomu zao Makao Makuu ya Chama, Kisiwandui, Unguja, Zanzibar.

“Kuanzia saa nne tunaanza utoaji wa fomu nanwapo baafhi ya watia nia wanaokuja kuchukua fomu ,”imesema

Aidha Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika atakuwa na kikao na watia nia wa ubunge na udiwani wa Kanda ya Pwani, itakayofanyika Hoteli ya Lions, Sinza, jijini Dar es Salaam.