Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula leo amefungua Mafunzo ya Makatibu wa Mikoa Na Wilaya Nchi Nzima katika ukumbi wa Halmashauri Kuu wa Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.
Pamoja na Mambo mengine ya msingi,Mangula amesema lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa juu maadhumuni na imani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) sanjali na mambo mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.
Aidha amesema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia jana na zaidi ya mada 17 zitafundishwa na wakufunzi mbalimbali waandamizi wa Chama na Serikali.
Mafunzo hayo yatahitimishwa Novemba 6, 2021 ambapo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga mafunzo haya.
More Stories
Dkt.bingwa wa watoto aikabidhi Hospitali ya Kanda Mbeya mashine mbili za kutoa dawa
Askari watatu wa TANAPA wafukuzwa kazi kwa tuhuma za rushwa
Wasira: CCM itashinda dola kwa kura si kwa bunduki