May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Aina mpya ya virusi vya Corona imegundulika ambavyo imeelezwa kuwa vinasambaa haraka zaidi na ni hatari kuliko virusi vilivyoleta ugonjwa wa COVID-19. Picha ya AP/New Scientist

BREAKING NEWS: Virusi vipya vya corona vyabainika, ni hatari zaidi, husambaa kwa kasi kuliko COVID-19

Na Mwandishi Wetu

Wanasayansi wamegundua aina mpya ya virusi vya corona ambavyo wanadai huenda vikasambaa kwa kasi zaidi duniani kuliko Covid-19 ambavyo bado vinaendelea kusumbua maeneo mengi duniani.

Hayo ni kwa mujibu wa utafiti mpya ambao uliongozwa na wanasayansi katika Maabara ya Kitaifa ya Los Alamos iliyopo New Mexico nchini Marekani.

Kwa mujibu wa watafiti hao, wamebaini kupitia sampuli mbalimbali kuwa, kati virusi hivyo vilionekana Februari huko Ulaya na vilianza kusambaa kwa haraka kwenda Pwani ya Mashariki ya Marekani na Machi, mwaka huu vilionekana kushika kasi zaidi.

Watafiti hao wamenukuliwa na gazeti la Los Angeles Times wakieleza kuwa, mbali na virusi vipya kuenea haraka, inaweza kuwafanya watu wawe katika hatari ya kuambukizwa mara ya pili baada ya kuugua ugonjwa kwa mara ya kwanza.

Ripoti ya utafiti huo yenye kurasa 33 ilichapishwa jana(Jumanne) katika mtandao wa BioRxiv, tovuti ambayo watafiti huwa wanaitumia kwa ajili ya kushirikishana kazi zao kabla ya kufanyiwa mapitio.

Hizo zikiwa ni jitihada za wanasayansi kuimarisha mshikamano katika kukabiliana na virusi vya COVID-19 hususani kutafuta chanjo au tiba.

Utafiti huo umetokana mlolongo wa vinasaba vya maumbile, ambao umebaini virusi hivyo vina uwezo wa kujibadilisha hali inayoweza kusababisha kuenea haraka na kufanya iwe vigumu kutibika.

Wanasayansi na mashirika makubwa yanayofanya kazi kwenye chanjo au dawa za kupambana na virusi vya corona wameiambia The Times kwamba, bado juhudi zinaendelea kwa kuwa, virusi hivyo ni changamoto, hivyo juhudi kubwa zinaendelea ili kujua njia za kuviangamiza.

HABARI HII KAMILI NA KWA KINA ITAKUWEPO KWENYE MAJIRA 07/05/2020