May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bandari ya Tanga yatarajia kuhudumia mizigo tani Mill 3

Na Hadija Bagasha ,timesmajira,Tanga

BANDARI ya Tanga inatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia tani Milioni 3,000,000 kwa mwaka kutoka Tani 750,000 za awali kwa mwaka baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Gati Mpya ambapo ujenzi wake kwa sasa unaendelea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na huduma za bandarini kuongezeka. 

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire wakati wa makabidhiano ya kupokea vifaa vya kuimarisha utendaji na ufanisi kwenye Bandari hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima vifaa vilivyotolewa ni mashine ya Crane 3 pamoja na Pilot Boti 1 Mpya.

Ngaire amesema uwepo wa vifaa hivyo na vitendea kazi utasaidia kuvutia biashara pamoja muda wa meli kukaa bandarini utapungua lakini pia itaongezeka matarajio ya mamlaka  kuongeza mapato yanayotokana na huduma zitakazokuwa zikifanyika kwenye Bandari hiyo sambamba na uongezaji wa vifaa vitakavyoongeza ufanisi ambao utakuwa na tija kubwa kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla. 

Alisema pia vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha utendaji kazi  na hata muda wa meli kukaa bandarini utapungua ikiwemo kuvutia biashara kutokana kwa wafanyabiashara ambao wanaitumia Bandari hiyo kupitisha shehena zao za bidhaa mbalimbali .

“Baada ya kupokea vifaa hivi ni kuimarisha utendaji kazi,  kuongeza ufanisi lakini hata muda wa meli kukaa bandarini utapungua uwepo wa vifaa hivi na vitendea kazi utavutia biashara kwani anapokuja mteja akakuta vifaa ni vichache inamdiscarage kwahiyo kuwepo kwa vifaa kutavutia biashara na watu wengi watapenda kupitishia mizigo yao hapa Tanga, Amesisitiza Ngaire. 

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema kwamba Serikali ya awamu ya Sita imekusudia kuifanya Tanga kuwa kitovu cha kusafarisha mizigo nje ya nchi na ndani ya Tanzania ipo pale pale na amekuwa akihimiza kila wakati.

Malima amesema kuwa Rais Samia ameliweka hilo na amekuwa akihimiza kila wakati kutokana na kutaka kujua maendeleo yake na akija yeye au makamu wa Rais au wakija viongozi wa kitaifa watawapeleka kwenye Bandari hiyo ili waweze kuona mafanikio makubwa ya  uwezekaji uliofanyika  kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote.

“Tunataka bandari ya Tanga kwamba watu wote wanaotaka kuleta mizigo duniani wakitaka kuipeleka Zambia, Malawi, DRC, Rwanda na Burundi kuwa wanapoinagalia bandari ya Mombasa, Dareslaam bandari ya Tanga iwe katikati kama bandari mbadala, “amesisitiza Malima. 

Alisema ili waweze kuwa na sifa hiyo ya viwango hivyo ni lazima wawe na huduma inayoendana na uwekezaji  unaofanywa na serikali hivyo wamekubaliana uwekezaji huo mkubwa wa kimakakti wenye thamani ya zaidi ya milioni 450 na kwamba kwenye bandari ya Tanga katika Gati linalojengwa amesisitiza liwe na huduma za kisasa.  

“Ni matarajio yangu kuwa  wakati yanafanyika hayo tupo kwenye mchakato wa uwekezaji wa Treni kuingia bandarini ili kuchukua mizigo hapo kupeleka Bandari ya Bandari Kavu Arusha.

Mkuu huyo wa mkoa amesema  watakaa kwa pamoja wajadiliane na wizara ya ujenzi ili  wafanye uwekezaji huo mkubwa wa mabilioni ya fedha Mkoani Tanga kwani wanahitaji nafasi ya kupumulia na nafasi hiyo ni Bandari kavu ya Arusha iliyopo eneo la Marula Arusha yenye ekari 200.

Malima amesema kwamba Novemba 20 mwaka huu inaingia meli ya Clinka tani elfu 50 itapakua mzigo na kula nje meli ya mafuta itaingia tani 49000 ukiachilia mizigo midogo na huo bado uwekezaji haujakamilika wanapokuwa nje wakija hapo mambo yatakuwa makubwa na itakuwa ndogo hivyo wameshauri mwishoni mwa mwezi watakutane na viongozi wa reli nchini,Bandari na Serikali ya Mkoa wa Arusha.

Mwisho.