May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Azam FC yasajili mshambuliaji mzoefu kutoka Zanaco

Na Mwandishi Wetu

UONGOZI wa Klabu ya Azam FC Dar es Salaam, jana imemtambulisha mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zambia, Rodgers Kola atakayekipiga kwa msimu ujao wa ligi akitokea Zanaco ya nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC, mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa amesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kudumu ndani ya klabu hiyo hadi mwaka 2023.

Akizungumzia usajili wa Kola, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema; Kola anakuja Azam FC kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/22″.

Amesema Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.