May 11, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Avunja rekodi duniani kwa kukutwa na uvimbe kilo 32

Mwanamke aliyekutwa na uvimbe mkubwa zaidi duniani, ni wa kilo 32

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online.

MWANAMKE mmoja nchini Mexico mwenye umri wa miaka 24, amekutwa na uvimbe wa kilo 32 ambao ulidumu kwa miezi kumi na moja ndani ya mwili wake.

Tukio hilo ambalo lilitokea mwaka 2017 na kutolewa uvimbe huo, madaktari walisema uvimbe huo ulikuwa mkubwa zaidi na ulitolewa bila kukwaruzwa.

Daktari alisema ” Hii ni hatua kubwa zaidi ambayo nimeifanyia kazi, uvimbe ulikuwa ni mkubwa sana hadi ukachukua asilimia 95 ya tumbo la mgonjwa huyo, ni mara chache sana kufanya kazi kwenye mfumo huu mkubwa ambapo uvimbe huo ulipima nusu ya kipenyo na mduara ukagundulika kuwa ni sentimita 157″ .

Kutokana na uvimbe huo, kulimfanya awe na shida ya kutembea, kupumua na kula kwa sababu ya kushinikiza kwa viungo vyake.

Dkt.Erik Hanson Viana, mwenye umri wa miaka 27, katika Hospitali Kuu ya Mexico, ndiye aliyefanya upasuaji huo ili kuondoa uvimbe.

Sasa, zaidi ya miezi sita, mwanamke anaweza kutembea tena na anaishi maisha ya kawaida.

Dkt.Hanson alisema mgonjwa alikuwa mzito, lakini baada ya kumfatilia afya yake aligundua mikono yake, miguu na uso wake unakuwa mwembamba lakini tumbo lake lilikuwa kubwa.

Alisema “Wakati nilikutana naye, aliweza kutembea hatua kadhaa kabla ya kushindwa kutembea ndipo nilipohisi alikuwa akipambana kupumua kwa sababu uvimbe ulikuwa ukiponda mapafu yake.

“Kama tungekuwa hatujafanya kazi ingekuwa imefika mahali ambapo asingeweza kutembea, na asingeweza kula.

“Ni ngumu kusema angeishi kwa muda gani, lakini ingekuwa hali mbaya ya maisha.”

“Siku mbili baada ya upasuaji alitoka hospitalini, tulipomuona miezi sita baada ya upasuaji kuona jinsi kidonda kilikuwa kinapona na kufuatilia shida zingine, alipona kabisa.

“Alikuwa amesimama sawa kabisa. Sasa anatembea kama mtu wa kawaida bila kuhitaji fimbo ya kutembea au vifaa vingine vya uhamaji na tumbo lake sasa liko sawa.” alisema.