Na Mwandishi wetu,Timesmajira SERIKALI imewahimiza wadau wa sekta binafsi, kampuni na wananchi mmoja mmoja kutumia fursa za uwekezaji zinazotolewa kupitia...
Penina Malundo
Na.Mwandishi weti,Timesmajira Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, ameanza kutekeleza...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, Agosti 5, 2026, ameshuhudia hafla ya utiaji saini wa Hati ya...
Na.Mwandishi wetu,Timesmajira Waziri wa Nishati,Deogratius Ndejembi, amesema Afrika ina fursa ya kutumia rasilimali zake za gesi asilia kuharakisha upatikanaji wa...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Wizara ya Nishati inaendelea kuhakikisha elimu kuhusu nishati safi ya kupikia inawafikia wananchi wa makundi mbalimbali ikiwemo...
Na.Mwandishi wetu,Timesmajira Serikali ya Awamu ya Sita imesema itahakikisha usalama na afya ya Watanzania wanaofanya kazi kwenye migodi ya dhahabu...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema Mkandarasi amekamilisha kwa mafanikio awamu ya kwanza ya kazi za uvutaji...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza kuwa lipo tayari kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153...
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Airtel Tanzania imeendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kimkakati na wateja kupitia mashindano ya Airtel Business Monthly Mug Tournament yaliyofanyika katika Klabu ya Gymkhana jijini Arusha, Tanzania. Mashindano hayo yaliwaleta pamoja viongozi wa biashara, wateja, na wadau mbalimbali, yakitoa fursa ya kujenga mahusiano yenye tija, kubadilishana mawazo, na kutambua fursa mpya za ukuaji wa biashara nje ya mazingira ya kawaida ya kikazi sambamba na kutambua na kuunga mkono mchezo wa Gofu nchini. Akizungumza wakati wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Airtel Business, Joseph Vipond, amesema Airtel inaamini ushirikiano imara hujengwa kupitia mawasiliano ya karibu na ushiriki endelevu, huku michezo ikitoa jukwaa bora la kuimarisha mahusiano hayo. Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano kwa Umma wa Airtel Tanzania, Sarah Nassor, amesema mashindano hayo yanaonyesha dhamira ya kampuni ya kujenga uhusiano wa kudumu na wadau kwa kuwashirikisha katika masuala yanayochochea mawasiliano, uaminifu, na ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Moja wa watumiaji wa huduma za Airtel ,Hiten Nathwani, ameipongeza kampuni ya Airtel kwa kuendelea kuboresha huduma zake sambamba na kuwasihi wachezaji Gofu hao kutumia huduma za Airtel.  Kupitia Airtel Business Monthly Mug Tournament, Airtel Tanzania inaendelea kuonyesha kuwa ushirikiano wenye tija hujengwa zaidi ya mahusiano ya biashara kwa kuunganisha watu toka sehemu mbalimbali na kuunganisha jamii ili kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi jumuishi wa kidijitali nchini.
Na Mwandishi wetu,Timesmajira Kampuni ya GF Vehicle Assemblers imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza...
