Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Askofu Allen Siso wa Jimbo la Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Tanzania Methodist Church, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Wilaya ya Kinondoni, amempongeza Mzalendo Alphonce Muyinga kwa jitihada zake za kujitoa kwa jamii na kueneza ujumbe wa amani unaolenga kuunganisha taifa.
Askofu Siso ameonesha kuguswa na mchango huo na kuamua kumuunga mkono Muyinga kwa kushiriki katika tukio la kizalendo litakalofanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Mei 8, 2026.
Tukio hilo linalenga kuigusa jamii kwa karibu zaidi huku likibeba ujumbe wa amani, uzalendo, na umuhimu wa kujenga umoja wa kitaifa miongoni mwa Watanzania.
Hatua hiyo inaonesha mshikamano wa viongozi wa dini katika kuunga mkono juhudi za wazalendo wanaojitolea kulinda na kuimarisha amani ya nchi, ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa.

More Stories
Mbarali yaweka mikakati thabiti kudhibiti mapato
Kihongosi aahidi kufuatilia upandishaji hadhi zahanati Masakta
DC,Chirukile ziarani Kongo kujenga mahusiano ya Kidiplomasia,uchumi