January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Arsenal yamsajili Nuno Tavares wa Benfica

LONDON, England

KLABU ya Arsenal imemsajili beki wa kikosi cha vijana

timu ya taifa ya Ureno U21, Nuno Tavares kutoka

Benfica.

Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni

usajili wa kwanza wa Arsenal msimu huu wa joto katika

makubaliano, wenye thamani ya pauni milioni 8,

Tavares, atajiunga na wachezaji wenzake huko kaskazini

mwa London mara tu atakapomaliza kipindi chake cha

kukaa Karantini.

Hata hivyo, Tavares ni zao la timu ya vijana ya Benfica

na amecheza jumla ya mechi 25 kwa klabu tangu

alipocheza kikosi cha kwanza kwenye Kombe la Super Cup

la Ureno dhidi ya Sporting Lisbon mnamo Agosti 2019.