May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Habari picha ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda akitoa taarifa ya uingiaji wa sukari kutoka Nchini India kwanjia ya magendo katika bandari ya Kigombe wakati wakiwa kwenye operesheni yao.Picha na Hadija Bagasha Tanga.

Akamatwa na mifuko 88 ya sukari ya magendo kutoka India

Na Hadija Bagasha Tanga,

JESHI la Polisi Mkoani Tanga linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Kigombe Mkoani Tanga kwa kosa la kumkuta akiwa na mifuko 88 ya sukari yenye kg 50 ambayo imeonekana kutenegenezwa nchini India ikiwa inaingizwa nchini kwa njia za magendo kwa kutumia bandari bubu ya kigombe akishirikiana na wenzake ambao walikimbia.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda alisema kwamba hatua ya kukamatwa kwa mkazi huyo ni kutokana na operesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazibiti biashara za magendo.

Kamanda Chatanda alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 17 Saa tisa mchana kwenye maeneo ya Mwarongo Kata ya Marungu Tarafa ya Pongwe ambapo wakiwa kwenye operesheni hiyo walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa na mifuko 88 ya sukari yenye kg 50 ambayo imeonekana kutenegenezwa nchini India ikiwa inaingizwa nchini kwa njia za magendo.

Kamanda huyo alitaja bidhaa nyengine ambazo zilikamatwa kuwa ni Madumu 45 ya Oili ya Magari yeye kg 20 kila mmoja na mifuko mitano ya mchele yeye ujazo wa kg 50 kila mmoja ikitokea nchini Pakistani.

Kamanda Chatanda alimtaja mtuhumiwa ambaye alikamatwa kuwa ni Hassani Tausilo aliyeshirikiana na wenzake ambao walikimbia na kutokomea kusikojulikana ambao kwa sasa bado wanasakatwa na jeshi hilo kutokana na kufanya biashara haramu ya magendo

“Sukari hii ilikamatwa inasafirishwa kwenye pikipiki tayari ilishashuhwa kwenye Ngalawa na kwenda kufichwa kwenye mapori yaliyopo kwenye kijiji cha Kigombe na kuanza kusafrisjwa kwa kutumia pikipiki ambazo pia nazo tulifanikiwa kuzikamata na mpaka sasa tunazishikia”Alisema kamanda huyo.

Alisema hivi sasa wanachoendelea nacho ni msako ulioanza kwenye mapori na kufanikiwa kukamatwa mifuko mengine 78 baada ya mifuko 10 kukamatwa kwenye pikipiki na mtuhumiw aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo naye alikimbia huku pia na mafumu 45 na huo mchele.