May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ramani ya Mkoa wa Shinyanga

Adakwa na polisi akidaiwa kumdanganya Waziri ana Corona

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MKAZI wa Kijiji cha Mwakitolyo eneo la Namba Mbili Wilaya ya Shinyanga, Mussa Kisinza (25) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwa Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee, Walemavu na watoto, Ummy Mwalimu akidai ana ugonjwa wa Corona.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba alimtaja mtuhumiwa aliyekamatwa mtuhumiwa huyo ambaye amekamatwa na askari wa Kikosi Kazi cha Makossa ya Mtandao mkoani Shinyanga Aprili 15 mwaka huu katika Kijiji cha Mwakitolyo wilayani Shinyanga.

Akifafanua Kamanda Magiligimba, alisema mtuhumiwa anadaiwa kumpigia simu, Waziri Ummy akidai yeye ameambukizwa ugonjwa wa COVID 19 ambapo baada ya taarifa hiyo, timu ya madaktari inayotoa huduma eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ilimtafuta mtuhumiwa huyo ili kumpatia huduma.

“Hata hivyo jambo la kushangaza na kusikitisha hakuweza kupatikana kutokana na kuzima simu yake ya kiganjani hivyo timu ya madaktari, iliyokuwa imekwenda eneo la tukio ilishindwa kumpata na kusababisha taharuki na hivyo Aprili 15, mwaka huu saa 1.00 asubuhi Kikosi Kazi cha Askari wa Makossa ya Kimtandao kilifika eneo la Mwakitolyo Namba Mbili.

“Kikosi hiki kilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anaendelea na shughuli zake katika machimbo ya dhahabu na kumpeleka katika Zahanati ya Kijiji cha Mwakitolyo, ili kuweza kubaini iwapo ni kweli anaugua ugonjwa wa COVID 19,” alisema.

Habari kamili pata katika gazeti la Majira…