Na Penina Malundo, Timesmajira
MCHUNGAJI Richard Hananja amelaani vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa dini kutumia majukwaa ya kidini kwa ajili ya kujitafutia umaarufu kupitia matukio ya utekaji au kupotea kwa watu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mchungaji Hananja alisema hakuna dini wala mtu mwenye maadili anayeweza kufurahishwa na matukio ya watu kutekwa au kupotea.
Amesema kuwa suluhu ya kweli ya changamoto hizo haiwezi kupatikana kwa maneno ya jukwaani bali kupitia vikao halali vya mazungumzo.
“Viongozi wa dini acheni kuishutumu serikali na vyombo vya ulinzi kwa tuhuma zisizo na msingi kwani vyombo hivyo vinafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.
“Natoa wito kwa Watanzania kuwa na subira na hekima, na kuepuka kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi,”amesisitiza.
Mchungaji Hananja alisema sababu ya chokochoko kuibuka ni pale uchaguzi mkuu unapokaribia kila taifa uwa kunakuaga na aina hiyo ya chokochoko kwani mara nyingi hali hiyo hutumiwa na baadhi ya watu kwa manufaa yao ya kisiasa.
“Tuwe makini na hawa watu kwani mwenendo huo unaweza kuhatarisha mshikamano wa kitaifa kupitia hao watu wenye manufaa yao binafsi ya kisiasa,tushikamane kulinda umoja na amani katika nchi yetu,”anesema.
Katika hatua nyingine, Mchungaji Hananja alisisitiza umuhimu wa mazungumzo kati ya pande zinazohusika, akieleza kuwa hata maandiko ya kidini yanahimiza matumizi ya “kiti na meza” kama njia ya kuleta suluhu ya kweli katika jamii.
More Stories
Matiko atangaza nia ya kugombea Ubunge Kivule
TPTC kuendesha kozi ya Walinda Amani wa Kirai
ACT wazalendo yaendelea kuteka watu