June 2, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi wa kike wapatiwa mafunzo ya tehama

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online

MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeeleza mafanikio yaliyopatikana katika kukuza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa wanafunzi wa kike nchini.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi Peter Mwasalyanga wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam .

Mhandisi Mwasalyanda amesema kwamba mwaka 2024/2025,mafunzo yamefanyika Aprili
kwa wanafunzi wa kike takribani 248,ambayo yanasaidia na kuhamasisha watoto
wakike kupenda masomo ya sayansi.

Pia amesema,shule za watoto wenye mahitaji maalum s‎hule 22,zitapatiwa vifaa vya TEHAMA ikiwemo
‎reader (machine za kisasa), Laptops, Embosser (printa ya nukta),runinga,braille machine (nukta nundu) orbit
‎nundu), digital voice recorders na magnifiers.

Pia ameeleza kuwa UCSAF inashirikiana na TBC kuboresha usikivu wa
‎matangazo yake,hivyo vituo 19 kujengwa kwa ruzuku ya zaidi ya bilioni 6.2.

Sanjari na hayo amesema Serikali kupitia mfuko huo imeboresha ofisi ya Msemaji wa Serikali,kwa kununua vifaa vya kisasa vyenye thamani ya milioni 200,huku lengo ni kuongeza ufanisi wa utoaji habari.

Pia amesema Serikali imeliwezesha shirika la Posta kwa kulipatia vifaa vya TEHAMA ili liweze kutoa huduma kidigitali.