March 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

STANBIC yaendelea kusaidia makampuni madogo ya uchimbaji mafuta na gesi

Na Penina Malundo,Timesmajira

BENKI ya Stanbic  imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Makampuni ya madogo ya Kitanzania yanayojishughulisha na uchimbaji wa mafuta na gesi katika kuwapa uzoefu katika miradi mikubwa ijayo.

Akizungumza hayo jana katika Kongamano na maonesho ya Petroli ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAPCE’25),Makamu wa Rais wa Miundombinu ya Nishati,Joe Mwakenjuki amesema wameona makampuni ya watanzania yakijitokeza katika kuangalia fursa mbalimbali katika miradi ya mafuta na gesi.

Amesema benki ya  Stanbic  imeweza  kusaidia makampuni hayo madogo ya kizalendo katika mnyororo wa thamani kwenye shughuli zao za  mafuta na gesi.

“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia  Kampuni ndogo za kitanzania katika kuwapa uzoefu katika miradi yao ya sasa wanayofanya ambayo ni midogo.

” Ni vema wenyewe kujipa uzoefu katika miradi ya sasa na sio kusubiri miradi mikubwa ya mafuta na gesi kufanya hata hii midogo wanaweza kufanya,”amesema.

Amesema watanzania wajitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa za miradi ya mafuta na gesi na kujiandaa na  miradi mikubwa zaidi kuliko wanayotekelezwa kwa sasa.

“Wanaweza kuja katika mabenki na kuweza kuwasaidia kupata uzoefu ili miradi mikubwa inapokuja  tutaweza kuwasaidia zaidi kwani mahitaji ya kifedha,amesisitiza.