Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
TAMASHA la Chakula la Coca-Cola Tanzania, maarufu ‘Kitaa Food Fest’ limehitimishwa jijini Dar es Salaam, kwa mafanikio makubwa huku maelfu ya wahudhuriaji wakifurahia ladha ya vyakula mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.
Tamasha hilo lililofanyika Jumamosi ya Novemba 23, mwaka huu, katika viwanja vya 710 Kawe, liliambatana na burudani ya muziki, mabalozi mbalimbali wa chapa ya Coca-Cola akiwemo pia mpishi maarufu kutoka Kenya na mcheza Rugby wa zamani Dennis Ombachi, anayejulikana kama ‘The Roaming Chef.’
Aidha, Tamasha hilo liliwaleta pamoja Mama na Baba Lishe zaidi ya 40 wa hapa nchini, ambao waliandaa vyakula mbalimbali vya asili ya Kitanzania, vilivyoambatana na vinywaji vya Coca-Cola ili kukamilisha mlo.
Mpishi maarufu kutoka nchini Kenya, Dennis Ombachi anayejulikana kwa mtindo wake wa kipekee wa upishi na haiba yake inayovutia kimataifa, alikuwa mmoja ya kivutio kikuu katika Tamasha hilo.
Ombachi alijiunga na wapishi maarufu wa hapa nchini katika mapishi na kuwa kivutio katika kuwahamasisha waliohudhuria kupitia ujuzi wake wa upishi.
“Uwepo wa Dennis Ombachi ulileta msisimko wa kipekee kwenye tamasha la mwaka huu,” amesema Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania.
“Ubunifu wake, pamoja na vipaji walivyojaaliwa wapishi wetu wa hapa nchini, vimelifanya tukio hili kuwa la kukumbukwa sana,” ameongeza.
“Tunajivunia kufanya Kampeni ambapo wapenda chakula na wapishi wanaweza kuungana, kusherehekea kwa pamoja. Tamasha la Chakula la Coca-Cola Kitaa Food Fest kwa mwaka huu limeweka viwango vipya kwa matukio ya upishi nchini Tanzania.”
Hata hivyo Tamasha hilo halikuhusu chakula pekee bali lilihusisha burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki pia.
Kwa upande wake Jonathan Jooste, Kaimu Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, amesisitiza lengo kuu la tamasha hilo lilikuwa kusherehekea utamaduni, mshikamano, na furaha ya watu kuwa pamoja.
“Tukio hili si kuhusu chakula kizuri pekee. Ni kuhusu kusherehekea utamaduni, mshikamano, na furaha ya watu kuwa pamoja wakifurahia chakula na vinywaji vya Coca-Cola,” amesema.
Mbali na hivyo pia, Wahudhuriaji mbalimbali walilisifu tamasha hilo kwa kuja kitofauti na kuwaleta pamoja wadau wa chakula kwa njia ya kibunifu.
Sherehe za tamasha hilo zilizojaa furaha ziliangazia dhamira ya Coca-Cola ya kuwaunganisha watu kupitia chakula na kukuza mahusiano ya kitamaduni yanayozalisha kumbukumbu za kudumu.
More Stories
Mzee wa Bwax afunika ‘Kitaa food Fest’ Mbagala
TBL yazindua Kampeni ya ‘Smart Drinking’
Msimu wa nne,tuzo za eagle entertainment, kufanyika kivingine