October 22, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mchengerwa: Hakuna Mtanzania atakayekosa matibabu

Na Penina Malundo,TimesMajira

WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, alisema kuwa kupitia huduma ya Afya kwa wote serikali imeendelea na itaendelea kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ni sehemu muhimu ya kuhakikisha mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote unakuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote mkoani Mtwara, amesema mpango huo ni ahadi ya taifa kwa kila Mtanzania, ikilenga kuhakikisha hakuna anayekosa matibabu kwa sababu ya kukosa fedha.

Mchengerwa amesema Serikali itashirikiana na mamlaka husika, jamii na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kubaini kaya zilizo katika mazingira magumu na kuhakikisha zinanufaika na mpango huo.

Amesema wananchi wenye uwezo watachangia gharama za bima kwa ajili yao na familia zao, huku Serikali ikiwasaidia wasioweza kumudu michango hiyo.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa familia zenye kipato cha chini na kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote.

“Kuanzia sasa, hakuna Mtanzania anayepaswa kukosa huduma za matibabu kwa sababu tu hana fedha,” amesema.

Uzinduzi huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata matibabu bila kukabiliwa na changamoto kubwa za kifedha.

Katika uzinduzi huo umeeenda sambamba na uzinduzi wa mikoa mingine nchini ikiwemo Mwanza, Mbeya, Arusha, Kigoma, Dodoma, Shinyanga, Tanga, Songwe, na Simiyu kwa wakati mmoja, ikimaanisha kuwa taifa zima limewasha mshumaa kwa pamoja kuashiria ushirikiano.