September 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenge wa Uhuru wafikia miradi 14 ya zaidi ya bil. 3.3 Kiteto

Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Kiteto

Mwenge wa Uhuru Kitaifa umetua Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara na kupitia jumla ya miradi 14 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 3.3.

Hayo yamebainishwa Julai 17,2024 na Mkuu wa Wilaya hiyo Remidius Emmanuel wakati akitoa taarifa yake,mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava,wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo na Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange.

“Mwenge wa Uhuru umepita katika Tarafa 2,Kata 4, Vijiji 5 na kukimbizwa umbali wa Km.67, ambapo jumla ya miradi 14 imefikiwa,” amesema Emmanuel.

Aidha amesema kati ya miradi hiyo mradi mmoja umezinduliwa, miradi 3 imefunguliwa na miradi 10 imekaguliwa

“Thamani ya miradi hiyo yote ni zaidi ya bil.3.3,ambapo kati ya fedha hizo jamii imechangia mil.4, Halmashauri ya Wilaya imechangia milioni 66.9 huku Serikali Kuu ikiwa imechangia zaidi ya bil.3,”amesema.

Aidha Mkuu huyo amefafanua kuwa wananchi wa Wilaya ya Kiteto katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 wamechangia jumla ya mil.69.7 vitu mbalimbali na n’gombe 4 na mbuzi 4, wenye thamani ya sh.mil.1.6.

” Kati ya fedha hizo sh.mil.67.7 zimetumika kugharamia manunuzi ya vifaa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambayo vimekabidhiwa kwa wahusika na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa eneo la mapokezi.