Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, usiku wa Oktoba 19, amejumuika na waumini mbali mbali wa Kiislamu katika Hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu wa Kikwajuni, nakufanyika katika viwanja vya Skuli ya Kisiwandui, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.
Alhaj Othman ambaye alikua ni Mgeni Rasmi wa Hafla hiyo, ameungana pia na Viongozi wa kitaifa wa Serikali, Dini, Jamii, Vyama vya Siasa na mamia ya Wananchi kutoka Maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Unguja.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watu wa Kikwajuni Sheikh Mohamed Suleiman Hibri na Katibu wa Jumuiya hiyo Sheikh Anas Omar Anas.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako