November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Miss, Mr walemavu wa kusikia kufanyika Julai 31

Penina Malundo, TimesMajira Online

KITUO cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania kimeaandaa mashindano Miss na Mr kwa walemavu wa kusikia ambayo yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Julai 31 mwaka huu katika ukumbi wa Serena.

Mkurugenzi wa Kituo hicho, Habibu Mrope ameuambia Mtandao huu kuwa, wameandaa mashindano hayo kwa lengo la kuliinua kundi hilo na kuwaona nao ni miongoni mwa watu wanaoweza kushiriki katika tasnia ya urembo.

Amesema, mashindano hayo kwa walemavu yanafanyika kwa mara ya kwanza hivyo wanaomba watanzania kuungana nao siku hiyo katika kushuhudia kinyang’anyiro hicho.

Mrope amesema, mashindano hayo yatawashirikisha jumla ya washiriki 24 kutoka Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Dodoma, Iringa, Tanga pamoja na Pwani na Dar es Salaam.

Amesema, baada ya kupata Mr na Mrs hao wataweza kushiriki katika mashindano ya nchi za Afrika ambayo yatafanyika Oktoba Mosi mwaka huu.

“Lengo kubwa ni kuhamasisha wadau wajitokeze katika mashindano hayo ambapo kiingilio kitakuwa sio kikubwa kwa Tanzania upande wa viziwi ni kundi la mwisho na haijawahi kutokea tangu uhuru hadi leo hatujawai kushiriki mashindano haya,”.

“Kupitia Mashindano haya yanatufanya tuingie na sisi kuonekana katika kundi ambalo lilisaulika katika mashindano hayo,mashindano kama haya tumekua tukiyaoma kwa jamii ya watu wanaosikia tu ndo wanaopewa nafasi lakini kwetu bado wanahofu kuhusu sisi viziwi kama tunaweza,”amesema

Amesema tunategemea vyombo vya habari kuhamasisha kwa ujumla hivyo tunaomba serikali itusaidia kupitia wizara yenye dhamana kushirikiana nao katika mashindano hayo.

Mrope alisema mashindano haya yanatarajia kuwa endelevu na kufanyika kila mwaka nchini kwa kushirikiana watu wenye ulemavu wa kusikia Mikoa yote.